Kocha mpya wa Simba Ljendari Abdallah Kibadeni “Mfalme Mputa” ambaye amerithi mikoba ya kocha Mfaransa kibabu, Patrick Liewig
Liewig hana lake tena Msimbazi, Kibadeni achukua mizigo yake
Na Baraka Mpenja
Siku
moja baada ya kocha wa wakata miwa wa Kaitaba, “Wanankulukumbi” klabu
ya Kagera Sugar, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ au Chifu
Mputa kuteuliwa kuwa kocha wa Simba hapo jana na leo hii kuanza kazi ya
kuifundisha klabu hiyo kwa kusaili wachezaji wa kuwasajili katika uwanja
wa Kinesi jijini Dar es salaam, Dar es salaam, klabu ya Kagera Sugar
imetangaza kumpata kocha mpya kutoka nchini Uganda.
Meneja wa kagera Sugar Hussein Mohamed ameiambia MATUKIO DUNIANI
kuwa walijua siku nyingi kuwa kocha wao Kibadeni alikuwa na mapenzi
makubwa sana kwa Simba na ndio maana walijiandaa mapema kutafuta kocha
mwingine.
Mohamed
amemtaja kocha huyo kuwa ni yule aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya
taifa ya Uganda wakati wa enzi za kocha Bob Wiliamson aliyewapa ubingwa
“The Cranes” mwaka jana, na anaitwa Mayanje Jackson.
“Mayanje
amewahi kuifundisha klabu yetu, aliondoka baada ya kuteuliwa kuwa kocha
msaidizi wa timu ya taifa, sasa anarejea tena na kila kitu kipo sawa”.
Alisema Mohamed.
Mohamed
alisisitiza kuwa Kibadeni alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na
amemaliza muda ake na Mayanje anajiandaa kusaini mkataba wa mwaka mmoja
siku za hivi karibuni.
Akizungumzia
suala la kuondoka kwa Kibadeni na athari zake kwa timu, Mohamed alikiri
kuwa Kibadeni ni kocha mzuri, ameacha pengo kubwa kutokana na uwezo
wake, lakini hawana uwezo kutokana na lejendari huyo kuwa na mapenzi
makubwa na Simba.
“Kibadeni
anaipenda Simba sana, aliichezea na kuifanyia makubwa, hakika katuacha
wakati tunamhitaji sana, tunamtakia kila la heri katika kazi yake mpya”.
Alisema Mohamed.
Pia
meneja huyo alisisitiza kuwa wanapanga mikakati ya usajili ili kupata
wachezaji wazuri wa kupambana na Kibadeni akiwa na Simba.
Katika
benchi la Ufundi la Simba, Kibadeni atakuwa anasaidiwa na walimu
wawili, Mganda Moses Basena na mzalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, wakati
Meneja atakuwa Nico Njohole na mtunza vifaa atakuwa Ally Cheche.
Mtihani
wa kwanza wa Kibadeni unatarajiwa kuwa nchini Sudan mwishoni mwa mwezi
ujao, ambako Simba itacheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe
la Kagame pamoja na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Simba
SC imepangwa Kundi A katika michuano hiyo pamoja na wenyeji El-Mereikh,
Elman ya Somalia na APR ya Rwanda, wakati Yanga ambao ni mabingwa
watetezi, wamepangwa Kundi C na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na
Vital ‘O’ ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC
wamepangwa kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman ya Somalia na
APR ya Rwanda.
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu
mjini Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B
pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy
ya Sudan na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Simba
SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, wakati
mabingwa watetezi, Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji Juni 20
kwa kumenyana na Express na mechi zote zitachezwa Elfashar.
0 comments:
Post a Comment