Na Baraka Mpenja
Michuano
ya Singaone Cup imeanza kushika kasi manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
kwa mchezo wa ufunguzi wa kundi A kupigwa leo hii.
Katika
mchezo huo klabu ya Bombili ilishuka ugani kumenyana na Soccer City na
kushuhudia City wakibuka kidedea baada ya kuwalaza wapinzani wao bao
1-0.
Kipute
hicho kimetajwa kuchezwa kwa ufundi mkubwa huku kila timu ikisaka
pointi tatu dakika hizi za mapema kwani ujanja ni kuwahi mapema.
Mdhamini mkuu wa mashindano hayo Bwana Golden Singaone ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Ruvuma (FARU) ameimabia MATUKIO DUNIANI kuwa ufunguzi wa mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka ulikuwa wa aina yake kutokana na watu wengi kujitokeza leo hii.
“Hakika
nimeridhishwa sana na mahudhuria ya wadau wa soka na mashabiki wote,
wamefika kwa wingi sana na kufanya mashindano ya mwaka huu yaanze kwa
kishindo”. Alisema Singaone.
Singaone
aliongeza kuwa mashindano hayo yanajumuisha timu za manisapaa ya Songea
tu, lakini anafikiria kuyapanua zaidi ili kuyafikia maeneo mengi zaidi.
“Ukiangalia
mikoa mingi soka linachezwa mjini, mimi nafikiri mkoani kwangu imefika
wakati wa kufuta suala hilo, nadhani nitajipanga kushirikiana na wadau
wengine kuyafikia maeneo yote ya Ruvuma”. Alisisitiza Singaone.
Mwenyekiti
huyo alisema licha ya yeye kuwa mwanasiasa ameamua kujiingiza katika
mchezo wa soka kwani unawavutiwa watu wengi zaidi duniani kote.
Baada
ya kipute cha ufunguzi leo hii baina ya Bombili na Soccer City,
Singaone alisema hapo kesho michuano hiyo itaendelea kwa timu za Kundi B
kushuka dimbani ambapo Nastboys watakwaana na Magereza majira ya saa
kumi kamili jioni.
Aidha Singaone aliwataka mashabiki wa soka kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kushangilia timu zao na kupata burudani ya soka.
0 comments:
Post a Comment