Na Baraka Mpenja wa
Wekundu
wa Msimbazi Simba “Taifa kubwa” chini ya kocha mkuu Mfaransa Patrick
Liewig leo hii majira ya saa 10 jioni watakuwa na kibarua kizito mbele
ya wanajeshi wa Charles Boniface Mkwasa “Master”, klabu ya Ruvu Shooting
katika uwanja wa Taifa ndani ya jiji la “Maji Chumvi”, Dar es salaam.
Kuelekea katika kipute hicho timu zote zimetamba kuibuka na ushindi, huku tambo za mashabiki zikiendelea kila kona ya jiji.
Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelu “Julio Alberto” ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa maandalizi ya mechi yamekamilika na kikosi chao kipo salama chini.
Julio
alisema kikosi cha Mnyama ambacho kimesheheni makinda wengi kitacheza
soka la kitabuni na kuwafurahisha mashabiki wao watakaofurika uwanja wa
taifa.
“Sisi
tunajenga kikosi na tunajua kwamba muda unahitajika, tunamshukuru Mungu
kwa kutupa uzima na kesho tutacheza kutafuta ushindi mnono mbele ya
Shooting ambao ni timu nzuri”.
Julio
aliongeza kuwa siku zote ukitaka kuona raha ya soka ukutane na Ruvu
Shooting ya Mkwasa kwani wanacheza soka safi na hapo kesho watakutana
wataalamu wa soka na kutoa burudani maridhawa.
Wakati
Julio akitamba kuwafunga Shooting, maafande hao kupitia kwa afisa
habari wake Masau Bwire wamesema kuwa kauli ya Simba kuwa wanataka
kulinda heshima yao kesho itagonga mwamba kwani watachinjwa tu.
Masau
alisisitiza kuwa wamejiandaa kwa uzuri sana na wanajua Simba wana
machungu ya kupoteza ubingwa na kuelekea kukosa nafasi ya pili, lakini
wamejipanga kupambana nao kupunguza machungu ya kushindwa kuwafunga
Oljoro mchezo wa nyumbani wiki iliyopita.
“Simba
sio timu ya kutubabaisha, wanajua soka la Ruvu shooting, mashabiki
wasikose taifa kesho, hakika kutakuwa na burudani kubwa sana, tuko fiti
sana kupambana na mnyama”. Alitamba Masau.
Simba
wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa nafasi ya nne ya msimamo
wakijikusanyia pointi 39 na Ruvu Shooting wanaofundishwa na Charles
Boniface Mkwasa wapo nafasi ya saba wakiwa na pointi 31 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment