Na Baraka Mpenja
Mabingwa
mara mbili mfululizo wa kombe la mapinduzi, makamu bingwa wa kombe la
kagame na ligi kuu msimu uliopita, klabu ya Azam FC “wana lambalamba”
ya jijini Dar es salaam chini ya kocha Mwiingereza Sterwat John Hall,
leo hii majira ya saa 11 jioni kwa saa za Morroco ambapo itakuwa saa
moja usiku kwa saa za afrika mashariki wanatarajia kushuka dimbani dhidi
ya AS FAR Rabat ya huko katika mchezo wa marudiano wa raundi ya tatu
kombe la shirikisho.
Mchezo
huo unatarajia kuwa wa kukata na shoka kutokana na uwezo mkubwa
walionao Azam pamoja na FAR Rabat, lakini matokeo ya mchezo wa kwanza
jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita uliomalizika kwa suluhu pacha
ya bila kufungana yanaweza kusababisha mechi ikawa ngumu zaidi.
Waarabu tabia yao inayojulikana sana ni kutafuta matokeo ya sare ama suluhu ugenini na kumalizia kibarua wakiwa kwao.
Wakiwa
Dar es salaam walifanikiwa kutumia mbinu hiyo na kulazimisha suluhu
mbele ya Azam, na leo hii wanatafuta njia ya kuwachinjia mbali wana
lambalamba wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania
bara wakijikusanyia pointi 48.
Katika
mchezo wa leo matokeo ya sare ya mabao yoyote ama ushindi utawapa
nafasi Azam kusonga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.
Kama
timu hizo zitaenda suluhu tena itatumika sheria nyingine kupata mshindi
wa kusonga mbele ambayo nikupigiana mikwaju ya penati ama matuta.
Azam
kwa kutambua fitina za waarabu ambao wanatabia ya kufanya umafia wakiwa
nyumbani kwao walienda huko mapema na kuweka kambi ya wiki moja ili
kuangalia mazingira ya huko na kuzoea mambo yao mapema.
Kuwahi
kwenda Morroco kumewapa nafasi ya kujua mengi na kujiandaa na mchezo
huo huku wakikabiliana na presha kubwa ya mashabiki wa Morroco wenye
hasira na Tanzania baada ya timu yao ya taifa kufungwa na Taifa stars
mabao 3-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia.
Leo
hii azam ikiwa na kikosi cha wachezaji mahiri kama Kipre Herman
Tchetche, John Rafael Bocco, Hamis Mcha “Vialli”, Abubakar Salum “Sure
Boy”, Jabir Aziz “Stima”, Brian Umony, Hamphrey Mieno, Himid Mao,
Michael Bolou , David Mwantika, na wengine wengi wana matumaini makubwa
ya kuwafunga wenyeji wao na kuwapa raha watanzania ambao kwa sasa
wamezoeza raha za Taifa stars.
Pia ufundi mkubwa wa kocha Hall unaweza kuwabeba matajiri hao wa Tanzania na kusonga hatua inayofuata.
Kila la Heri Azam Fc, Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Azam fc.
0 comments:
Post a Comment