Na Baraka Mpenja
Mtunzi wa
kitabu cha kwanza kutokea Tanzania kinachozungumzia soka la Tanzania
kiitwacho “SOKA LA TANZANIA”, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kitabu
chake kimepokelewa vizuri na wadau wa soka hususani siku ya mechi ya
watani wa jadi, Simba na Yanga mei 18 mwaka huu uwanja wa Taifa ambapo
Simba walichezea kichapo cha mabao 2-0.
Mwakalebela ameimbia MATUKIO DUNIANI
kuwa kitabu hicho kwa sasa kimeshasambazwa jiji zima la Dar es salaam
“Jiji la maji chumvi” na sasa wanaanza mipango ya kukisambaza mikoani.
“Kila kona
ya Dar es salaam kitabu hiki kimefika madukani, sasa tunajiandaa
kukipeleka katika mikoa mbalimbali ili wadau wapate kukisoma kwa kina na
kujifunza mambo mengi kuhusu soka la Tanzania”. Alisema Mwakalebela.
Zoezi la
kukisambaza mikoani linaweza kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo na kila kitu
kinakwenda sawa hivyo wapenda soka wakae mkao wa kula.
Katibu
Mkuu huyo wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), na mdau
mkubwa wa kandanda Fredrick Mwakalebela alisema kitabu hicho gharama
yake ni shilingi elfu kumi tu (10,000.
Mwakalebela
alisisitiza kuwa kila anayependa maandeleo ya soka la Tanzania ni
nafasi yake kutafuta nakala ya kitabu hiki kwani ni muhimu sana kwa
kweli.
“Kitabu
kinazungumzia soka la vijana, wanawake, mpango wa rais Dkt. Kikwete
kuendeleza soka letu, masuala ya makomandoo wa uwanjani, matatizo
mbalimbali ya soka la Tanzania na nini kifanyike, hayo ni miongoni mwa
mambo mazuri yanayopataikana katika kitabu hiki”. Alisema Mwakalebela.
Pia
alisema amepokea pongezi nyingi sana kutoka kwa wadau kitu ambacho
anaamini kuwa watu wanakipenda kitabu na wataendelea kukipenda zaidi.
Pia kitabu
hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, wadhamini, uhusiano
kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa
miguu Tanzania.
“Pia
nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi
cha miaka minne nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa
makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa
kwanza Juni 15, 2006,”. alisema Mwakalebela.
0 comments:
Post a Comment