|
|
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Supersport.com
Kocha
wa timu ya taifa ya Nigeria “Super Eagles” na mabingwa wa soka barani
Afrika,Stephen Keshi amesema anapendelea sana na kuweka umakini mkubwa
katika mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini
Brazil kuliko kombe la shirikisho linalosimamiwa na FIFA ambalo
litafanyia Barzili pia.
Keshi
ambaye yuko na kikosi chake mjini Nuremberg nchini Ujerumani akijiandaa
kuvaana na timu za taifa za Kenya na Namibia katika mechi za kuwania
kufuzu kombe la dunia zitakazopigwa mwezi juni mwaka huu alisisitiza
kuwa kombe la shirikisho ni zuri lakini FIFA World Cup ndio kila kitu
kwake.
The
Super Eagles atacheza kombe la shirikisho baada ya kutwaa ubingwa wa
Afrika mwanzoni mwa mwaka huu nchini Afrika Kusini, huku waliokuwa
mabingwa watetezi, Zambia wakitolewa mapema hatua ya makundi.
Keshi aliulizwa hivi: Endapo
utapewa nafasi ya kuchagua sasa, Kombe la shirikisho au kuwania kufuzu
fainali za kombe la dunia, ungechagua nini?
Alijibu
bila hata kigugumizi, “Nitachagua mechi za kuwania kufuzu kombe la
dunia muda wote. Kweli, kombe la shirikisho ni zuri sana, lakini kamwe
huwezi kulifafanisha na kombe la dunia, hakika FIFA World Cup ni kombe
la heshima kubwa mno”.
Keshi atakuwa amejifunza sana
kwa mabingwa wa Zamani wa Africa, MAFARAO wa Misri ambao waliwekeza
nguvu kubwa zaidi katika kombe la shirikisho mnamo mwaka 2009 nchini
Afrika kusini, lakini wakasahau kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu
fainali za kombe la dunia na kutolewa na wapinzani wao wakubwa Algeria.
“Tutalipa uzito wa kutosha kombe la shirikisho, lakini ni lazima mwakani
turudi tena Brazil tukiwa moja ya wawakilishi wa Afrika katika michuano
ya kombe la dunian”. Alisema Keshi.
0 comments:
Post a Comment