Na Baraka Mpenja
Tabia
ya timu za ligi kuu soka Tanzania bara kupuuza mazoezi ya maandalizi ya
mechi zao za mwisho kwa madai kuwa hazishuki daraja wala hazihitaji
ubingwa inaua ushindani wa ligi na kushusha kiwango cha timu hizo.
Akihojiana na mtandao wa MATUKIO DUNIANI,
katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Fredrick
Mwakalebela amesema kuwa timu za ligi kuu zinatakiwa kuachana na kusumba
hii ambayo ni sumu mbaya kwa soka letu.
“Ukiangalia
ligi za wenzetu ligi inajigawa kama Tanzania, kuna timu zinahitaji
ubingwa, nyingine zinahitaji nafasi za juu, wakati kundi la mwisho
wanahitaji kukwepa mkasi wa kushuka daraja, lakini ukiangalia mechi
zinazowakutanisha wasioshuka daraja wala hawahitaji ubingwa na wale
wanaohitaji ubingwa au wanashuka daraja, ushindani uko pale pale”.
Alisema Mwakalebela.
Mwakalebela
alisema kujenga historia ya timu kufanya vizuri katika michezo yote ni
muhimu sana na timu za Tanzania zinatakiwa kuwa na malengo ya kujenga
jina na kuwajenga wachezaji wao kushindana katika mechi zote ili wapate
nafasi ya kuonwa na walimu wa timu za taifa pamoja na timu za nje ya
Tanzania.
“Mchezaji
anatakiwa kucheza katika kiwango chake cha siku zote bila kujali
anacheza mechi gani, kama watazembea kwa madai kuwa hawashuki daraja
wala kupata ubingwa, hakika ni ufinyu wa mawazo”. Alisema Mwakalebela.
Pia
katibu huyo wa zamani wa TFF aliongeza kuwa viongozi wa timu za Tanzania
wanatakiwa kujua kuwa timu inahitaji maandalizi ya muda mrefu na
kushindana katika michezo yote, hivyo waache tabia ya kuwapumzisha
wachezaji kwa muda mrefu kwa madai kuwa hata wakifungwa hawaathiriwi na
matokeo hayo.
Siku chache zilizopita mtandao wa FULLSHANGWE
ulihojiana na baadhi ya makocha wa timu za ligi kuu kuhusiana na
maandalizi yao ya michezo ya kufunga pazia la ligi kuu mei 18 mwaka huu
na walieleza kuwa kwa muda mrefu hawapo kambini kwa sababu mechi ziko
mbali na kizuri hawataki ubingwa wala hawashuki daraja.
Historia ya klabu ni kitu cha msingi, ni muhimu kwa timu kujiandaa katika mechi zote.
0 comments:
Post a Comment