

Na Happiness Mnale


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa, leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku tisa ya ujenzi na
kukagua uhai wa chama hicho katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa
wa Manyara.
Dk. Slaa ataambatana na watendaji wa makao makuu ya chama sambamba na wabunge wote wa CHADEMA Mkoa wa Manyara.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa
CHADEMA, Tumaini Makene, ilieleza katika ziara hiyo, mbali ya kupokea
taarifa na kukagua uhai na ujenzi wa chama hicho, Dk. Slaa pia atafanya
mikutano ya hadhara miwili pamoja na mikutano ya kikazi ya ndani, ambapo
atakutana na wanachama na viongozi wa maeneo husika.
Makene alieleza kuwa siku ya leo, Dk. Slaa atafanya mkutano Babati
mjini katika viwanja vya Kwaraa na atapokea salamu za wananchi wa eneo
la Mnjingu.
Makene pia alieleza kesho Dk. Slaa ataelekea Hanang, ambapo atapita na
kuwasalimia wananchi wa vijiji vya Masqaloda, Measkron, Nangwa na
Dirma, kabla ya kufanya mikutano ya hadhara Balangida na Gendabi mjini
Hanang.
Pia alieleza Mei 20 na 21 Dk. Slaa atafanya mikutano ya hadhara Basutu
na Haydom iliyopo Mbulu, na mkutano mwingine atafanya Dongobesh na
Mbulu mjini.
“Mei 22, 2013 akiwa njiani kuelekea Babati Vijijini, Katibu Mkuu
atawasalimia wananchi wa vijiji vya Mutuka na Mwikansi kabla ya kufanya
mkutano wa hadhara Galapo, Babati Vijijini, kuanzia saa 8 mchana na Mei
23, 2013 atakuwa na mikutano ya hadhara maeneo ya Riroda, Dareda na
Bashnet, Babati Vijijini,” alieleza Makene.
Aidhamwaka huu Dk. Slaa atakuwa Simanjiro na atafanya mikutano ya
hadhara katika maeneo ya Msitu wa Tembo, Ngorika, Ngage, Orkesimet,
Namaruru kisha atamalizia na Mererani.
IMECHOTWA GAZETI LA TANZANIA DAIMA LEO
0 comments:
Post a Comment