Thursday, May 2, 2013

Menja wa bia ya serengeti Bw Allan Chonjo akimkabidhi bw.Amadeus Minja jenereta aliojishindia kuopitia promosheni inyoendeshwa na kampuni ya bia ya serengeti
 Zaidi ya milioni mia saba ya zawadi kushindaniwa (700ml) kupitia bia yake bora ya Serengeti Premium Lager!
Mei 2, 2013, Dar Es Salaam: Kampuni ya bia ya Serengeti katika juhudi zake za kutambua na kuthamini wateja wake, leo imezindua promosheni ambayo inaendana na kampeni yake kuu inayoendelea ya TUPO PAMOJA.  Tupo Pamoja ni kampeni inayotambua wateja na kusherehekea nao pamoja.
Mteja anaweza kujishindia kuanzia shilingi elfu kumi hadi million moja na pia anaweza kujipatia bia ya bure papo hapo.  Kampeni hii inatarajiwa kuendeshwa kwa miezi mitatu ijayo.
Katika promosheni hii ya winda na ushinde, mteja atakaponunua bia ya  Serengeti ataweza kupata maelezo chini ya kizibo kama ilivyokuwa katika kampeni iliyopita ya vumbua hazi na chini ya kizibo.   Atapata namba maalum ambayo atatuma kwa njia ya sms kwa namba maalum na papo hapo atapata ujumbe utakaomjulisha ameshinda kiasi gani au kama amejipatia bia ya bure.   
Kama kawaida ili kuhakikisha ushindi huu ni waukweli na uhakika, promosheni hii itasimamiwa na bodi ya Bahati nasibu, kampuni maahiri ya PWC na itaendeshwa na Push Mobile.
Akiwakaribisha wageni na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuzindua promosheni hii ya Winda na Ushinde iliyofanyika katika kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar Es Salaam, Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru alisema kwamba bia ya Serengeti lager ni bia inayojali na kuwatambua wateja wake kwa kiasi kikubwa. 
“Kampeni na promosheni zetu zinalenga haswa kuwashukuru na kuwanufaisha wateja wetu,Winda na Ushinde itabadilisha maisha ya watu wengi.  Bia hii inatambua umoja na ushirikiano uliopo baina yetu na hivyo basi, tunazindua promosheni ambazo zawadi zake ni utoaji wa kweli na kuwafanya wateja wetu kujisikia kwamba wanadhaminiwa kwa njia moja au nyingine.,”alisemaBw. Mafuru.
Uzinduzi wa promosheni hii pia ulihudhuri wa na Mkurugenzi mkuu (Group Managing Director) Bw.Charles Ireland na Mkurugenzi mkuu wa Masoko na Ubunifu (Group marketing and Innovation Director) Ms. Debra Mallowah.
Wengine waliohudhuria ni Maofisa kutoka bodi ya Bahati Nasibu, maofisawa PWC na Push Mobile.  Pia kutoa walihudhuria washindi waliowahi kushinda zawadi mbalimbali katika promoshen za nyuma. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video