Na Baraka Mpenja
Wanalizombe
Maji Maji FC ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajiwa kufanya uchaguzi wa
viongozi mwezi ujao ili kuendeleza gurudumu la kuirudisha timu hiyo soka
la ushindani zaidi.
Mwenyekiti
wa kamati ya uchaguzi Joseph Mapunda amesema leo hii kamati yake
iliyochaguliwa kuhalali na viongozi wa timu hiyo wanakaa kikao ili
kujadili ni lini zoezi la uchukuaji wa fomu litaanza, usaili wa wagombea
na siku ya kufanya uchaguzi.
“Nafurahi sana kuongea na watu wa Mtandao wa MATUKIO DUNIANI,
ninapenda kutumia nafasi hii adimu kuwataarifu kuwa mchakato wa
uchaguzi unakwenda sawasawa na leo hii majira ya jioni tutatoa utaratibu
mzima”. Alisema Mapunda.
Mapunda alizitaja nafasi saba kuwa ndio zitawaniwa na wanachama halali wa klabu hiyo.
“Kuna
nafasi mbili za juu, mwenyekiti na makamu mwenyekiti pamoja na nafasi
za wajumbe watano wa bodi ya timu, nadhani watapatikana mwezi ujao kama
mambo yatakuwa mazuri”. Alisema Mapunda.
Pia mwenyekiti huyo alisema mchakato wa uchaguzi utazingatia haki sawa kwa wote, hakuna mgombea atakayeonewa.
“Kwa
uzoefu wangu wa kusimamia uchaguzi, sina wasiwasi kabisa kama kuna
ujanja ujanja utafanyika, watapita wenye sifa zinazotakiwa, nataka
wanachama wa Maji Maji watambue kuwa tupo kwa ajili ya kuendeleza klabu
yetu nzuri”. Alisema Mapunda.
Mapunda
alisema wanawakaribisha watu wote kuomba nafasi za uongozi katika klabu
yao, hata kama mtu ni mwenyeji wa Ruvuma halafu anaishi nje ya mkoa wa
Ruvuma anakaribishwa sana kuomba nafasi.
Pia
aliwataka wanachama wa klabu hiyo kuwa makini wakati huu wa kutafuta
viongozi wa kuiongoza klabu yao, kwani kama watafanya makosa basi
wataendelea kuirudisha nyuma.
0 comments:
Post a Comment