Saturday, May 4, 2013

Kalusha Bwalya @ SS com

Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Supersport.com
Rais wa chama cha soka nchini Zambia FAZ Kalusha Bwalya amefurahiswa na kurejea kwa michuano ya ukanda wa nchimwanachama wa baraza la michezo kusini mwa Afrika COSAFA ambayo itafanyika mwaka huu nchini Zambia.
Kalusha alisema michuano hiyo mikubwa itawasaidia wachezaji wa ukanda huo kushindana kwa nguvu, na Zambia kupewa heshima ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo hakika ni heshima kubwa sana kwao.
“Nimefurahishwa na urejeo wa michuano hii, zambia kuwa mwenyeji ni furaha kubwa sana, tumesubiri sana nafasi hii na kuwa mwenyeji imetupa heshima zaidi”. Kalusha ameuambia mtandao wa Superspot.com
Pia aliongeza kuwa michuano hiyo itatoa nafasi kwa wachezaji kushindana kiundugu sanjari na kujulikana kutokana na michuano hii kurushwa na vituo mbalimbali vya runinga.
Kalusha alikuwa miongoni mwa wasemaji wakuu wa COSAFA katika draw iliyofanyika jijini Lusaka nchini Zambia.
Katika michuano hiyo timu ya taifa ya Tanzania “Taifa stars” imealikwa kushiriki na COSAFA na tayari shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limekubali mwaliko huo muhimu ambao utawakutanisha wachezaji wa Tanzania na wachezaji wengine wa Kusini mwa Afrika.
Stars itaenda kucheza michuano hiyo ikiwa tayari ilishakutana na Zambia waliokuwa mabingwa wa soka barani Afrika kabla ya kuupoteza mwaka huu nchini Afrika kusini na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 liliLofungwa na Mrisho Ngasa uwanja wa taifa mwezi Disemba mwaka jana.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video