Baadhi
ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walioshiriki katika
Mkutano wa Jumuiya za UVCC, UWT na Wazee. Mkutano huo uliofanyika Makao
Makuu ya CCM Zanziba Kisiwandui. Mwandishi
wa Gazeti la Habari Leo Khatib Burecha akiuliza swali katika Mkutano wa
Waandishi wa habari na Jumuiya za UVCC, UWT na Wazee. Mkutano huo
uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanziba Kisiwandui
Naibu
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib
akifafanua jambo katika Mkutano wa Jumuiya za UVCC, UWT na Wazee na
Waandishi wa habari. Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya CCM Zanziba
Kisiwandui
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Jumuiya
za Chama cha Mapinduzi UVCCM, UWT na Wazazi zinakusudia kuwajengea
uwezo Vijana ili kujinasua na hali ngumu ya kimaisha kwa kuwasomesha
kupitia Skuli za Wazazi na Elimu ya Amali ili waweze kujiajiri wenyewe.
Zimesema
Vijana watakapopata Elimu hiyo itawasaidia kuweza kujiajiri na
kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira linaloendelea hapa Nchini.
Naibu
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania UWT Salma Abuod Talib
ameyamesa hayo huko Makao makuu ya CCM Zanzibar Kisiwa nduwi alipokuwa
akizungumza na Waandishi wa habari kwa lengo la kupongeza mafanikio ya
ziara ya kichama iliyofanywa na Dkt. Shein.
Amesema
Mafunzo ya Amali yatawasaidia Vijana kuondokana na fikra za kutegemea
Ajira kwa Serikali na kuwawezesha kujiajiri wenyewe badala ya kutegemea
Serikali.
Akizungumzia
ziara hiyo Bi Salma amesema ziara ya DKT Shein imekuwa na mafanikio
makubwa kwani imeweza kuongeza Wanachama wapya jambo ambalo ni ishara
ya wazi ya uhai na matumaini ya ushindi wa Chama hicho katika Chaguzi za
badae .
Amesema
katika hali hiyo kuna haja kubwa kumpongeza kiongozi hiyo kwani imetoa
picha ya kufanikiwa kukiimarisha chama na kukiletea maendeleo hapa
visiwani na Tanzania kwa ujumla.
“Jumuiya
za chama cha mapinuzi (UVCCM , UWT na Wazazi) Tuna mpongeza kwa dhati
kabisa kuwa Mjasiri wa kutembea bila kuchoka na kuwa tayari kutumika
kila ambapo alitakiwa ushiriki wake, inaonesha wazi kuwa Makamu
Mweneyekiti wetu ni mtu wa watu na anapenda watu pamoja na maendeleo
yao”amesema Bi Salma.
Aidha
alisema katika ziara hiyo DKT Shein alikagua na kutembelea miradi ya
CCM ambapo miradi 35 iliwekewa jiwe la msingi na kuziduliwa ikiwemo
SACCOS mbali mbali na Vikundi vya Ushirika .
Akizungumzia
sintofahamu iliyopo katika baadhi ya Majimbo Bi Salma alisema CCM
imepanga kufanya vikao vitakavyojumuisha Viongozi wa Majimbo wakiwemo
Wabunge na Wawakilishi pamoja na Wananchi wao ili kuimarisha uttendaji
wao
Amesema
Vikao hivyo vitatoa mustakabali nzuri kwa Viongozi hao na kuweza
kuwatumikia Wananchi waliowachagua katika hali inayofaa.
Jumla
ya Wanachama wapya 5,448 kutoka Vyama mbali mbali vya Siasa wamejiunga
na Chama cha Mapinduzi kufuatilia Ziara ya Makamo Mwenyekiti wa Chama
hicho Dkt. Ali Mohammed Shein aliyoifanya karibuni kutembelea Mikoa
mitano ya Unguja na Pemba kwa lengo la kuangalia na kukipa uhai chama
cha Mapinduzi na jumuiya zake.
0 comments:
Post a Comment