Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Miamba
ya soka la Hispania Real De Madrid na wazee wa Katalunya wanaiwinda kwa
nguvu zote saini ya nyota wa Chelsea Mbrazil David Luiz.
Mbrazil huyo anaweza kuwa lulu mbele ya kocha mpya anayekuja Chelsea,
Jose Mourinho ambaye amevutiwa na uwezo wake katika nafasi ya ulinzi.
Luiz
aliigharimu Chelsea Pauni Milioni 21 na kama wanataka kumuuza basi
watahitaji faida zaidi ili kunufaika na nyota huyo mwenye uwezo mkubwa
wa kucheza safu ya Ulinzi.
Mourinho anataka beki mpya wa kati, kiungo mkabaji na angalau mshambuliaji mmoja katika kurejea kwake Stamford Bridge.
Luiz amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji chini ya Rafa Benitez na imemsaidia kupunguza makosa yake wakati anacheza kama beki.
Chelsea
imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji anayetakiwa na Liverpool,
Krygiakos Papadopoulos wa Schalke, lakini inamchukulia kinda huyo wa
miaka 21 kama ghali sana.
Mourinho
ni shabiki mkubwa wa Raphael Varane wa Real Madrid pia, lakini suala
hilo litaingiliwa na siasa zake za kuondoka Bernabeu.
Tayari, wanaonekana kuimarisha safu yao ya ulinzi wakiwa na Branislav Ivanovic ambaye pia anawezwa kuhamishiwa beki ya kulia.
Mashine ya Kweli: Beki wa Chelsea, David Luiz alisajiliwa kwa Pauni Milioni 21 kutoka Benfica
Nyota: Luiz alikuwa na mchango mkubwa wakati Chelsea inatwaa Europa League
Kipaji: Raphael Varane wa Real Madrid (akipiga juu) anakubalika mno mbele ya Mourinho
Kazi ya kwanza ya Jose Mourinho Chelsea itakuwa kuimarisha safu ya ulinzi
Madrid
itakijenga upya kikosi cha Mourinho kupitia kwa Carlo Ancelotti.
Watakuwa tayari kumuuza beki Pepe kuliko Varane na Manchester City
wamepewa ofa ya kumsajili beki huyo Mreno kwa Pauni Milioni 20.
Kwa
upande wao, Barcelona wanapambana kuwania saini ya beki wa kati ambaye
hatazidi Pauni Milioni 25. Luiz yumo kwenye orodha yao muda mrefu,
lakini si kipaumbele cha mwanzoni.
Mourinho atatakiwa kuamua mustakabali wa John Terry na Frank Lampard msimu ujao
Walimtaka
Thiago Silva kutoka Paris St Germain, lakini ni ghali mno wakati
Manchester City hawako tayari kumuuza Vincent Kompany. Barca inamtaka
beki kinda wa Roma, Marquinhos lakini anaweza kuwa tayari kubaki kwa
msimu mwingine Italia.
Thomas
Vermaelen wa Arsenal anaweza kurejesha makali yake, lakini kumaliza
kwake msimu vibaya kunamfanya Luiz awe midomoni mwa watu zaidi yake.
Thomas Vermaelen amekuwa akimulikwa na Chelsea
0 comments:
Post a Comment