Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Licha ya
kutokushuka daraja wala kuwania ubingwa ambao tayari upo mikononi mwa
Yanga msimu huu, maafande wa JKT Oljoro wa jijini Arusha wametamba
kuonesha kabumbu maridhawa kesho kutwa katika uwanja wa Shekh. Amri
Kaluta Abeid dhidi ya Azam Fc kutoka Dar es salaam.
Kocha msaidizi wa maafande hao Riziki Shawa ameimabia MATUKIO DUNIANI
kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na lengo lao ni kutoa burudani kubwa
kwa mashabiki wao ambao wamewaungana mkono sana msimu huu.
“Awali ya
yote tunamshukuru Mungu aliyetupa uzima mpaka siku ya leo, sisi
tumejiandaa vizuri kuwavaa Azam, mchezo utakuwa mzuri sana”. Alisema
Shawa.
Kocha huyo
alisema mchezo huo hauna mchecheto mkubwa sana kwani wao hawashuki
daraja wala hawahitaji ubingwa, kikubwa wanahitaji burudani na kupata
ushindi wa kuhistoria.
“Azam ni
timu nzuri, imetoka kucheza mashindano ya kimataifa na wanajiamini
zaidi, sisi Oljoro hatuna wasiwasi kutokana na maandalizi yetu”.
Shawa
aliwataka mashabiki wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo
kwani wamejiandaa kuonesha kandanda la kufa mtu na kila atayekuwepo siku
ya mechi uwanjani hatajuta kutoa kiingilia kutazama mechi hiyo.
Kocha huyo
mwenye historia ya kulijua soka la Tanzania aliongeza kuwa wakishinda
watafikisha pointi 32 na hii itatoa nafasi nzuri ya kujipanga zaidi
msimu ujao ili kupata nafasi tatu za juu.
Pia Shawa alisisitiza kuwa katika mchezo huo watawatumia baadhi ya vijana wao ambao wanaamini wataleta ushindani mkubwa.
0 comments:
Post a Comment