Mshambuliaji wa klabu ya PSG
ya Ufaransa Jeremy Menez amefungiwa mechi nne kwa kosa la kumtukana mwamuzi
wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza(Ligue One) mwezi uliopita.
Chama cha soka nchini Ufaransa
kimedokeza kuwa mchezaji huyo alimtukana mwamuzi huyo mara tu baada ya
kuoneshwa kadi nyekundu.
Hata hivyo mchezaji huyo
atalazimika kusherehekea ubingwa wa ligi pamoja na mashabiki wake jukwaani
watakapoialika Stade Brest katika mchezo wa ligi Jumamosi wiki hii.
Adhabu yake inataraji kuanza
wiki ijayo huku akilazimika kuwa nje ya dimba kwa mechi tatu za kwanza msimu
ujao.
Menez alikuwa shujaa wa
mechi dhidi ya Olympic Lyon kwa kuifungia goli la pekee lililowapatia ubingwa
wa ligi msimu huu.
0 comments:
Post a Comment