JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu: +255-22-2112035/40 | S.L.P. 9223 | |
Nukushi: +255-2122617/2120486 | Dar es Salaam | |
Barua pepe: [email protected] | ||
06 Mei 2013 |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa
kutumia madaraka aliyopewa chini ya Kifungu cha 3(2) (a) cha Sheria ya
Bodi ya Parole Sura 400 amemteua Jaji Mstaafu Eusebia Nicholaus Munuo
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kuanzia tarehe 24 Aprili,
2013. Mheshimiwa Eusebia Nicholaus Munuo ni Jaji Mstaafu wa Mahakama ya
Rufani Tanzania.
Sambamba
na uteuzi huo Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kutumia
madaraka aliyopewa chini ya kifungu 3(2)(f) cha Sheria hiyo, amewateua
Bw.John William Nyoka na Bw. Fransis Stolla kuwa wajumbe wa Bodi hiyo.
Bw. John William Nyoka ni Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu na kabla ya
kustaafu kwake alikuwa Mshauri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
nchini Namibia kama Mshauri wa Magereza na Bw. Fransis Stolla ambaye ni
Wakili wa Kujitegemea na kwa sasa ni Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika(Tanganyika Law Society).
Wajumbe
hawa pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka, Mkemia Mkuu wa Serikali,
Kamishna wa Ustawi wa Jamii na Mjumbe mmoja kutoka Ofisi ya Rais ndio
wanaounda Bodi ya Taifa ya Parole kwa mujibu wa kifungu cha 3(2) cha
Sheria hiyo.
Mbarak Abdulwakil
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
0 comments:
Post a Comment