Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Beki
wa Chelsea Branislav Ivanovic amevunja ukimya wake juu ya kitendo
alichofanyiwa na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez cha kung`atwa
mkono wake mwezi uliopita.
Suarez
alifungiwa mechi 10 na chama cha soka nchini Uingereza baada ya kufanya
kosa hilo katika mechi ya ligi kuu iliyomalizika kwa sare ya 2-2 dimba
la Anfield.
Ivanovic alisema alishangazwa na tukio lile la utata kwake, lakini amemsamehe Suarez na waendelee na mambo mengi ya kimaisha.
NILISHANGAA: Branislav Ivanovic amesema binafsi hakutarajia kufanyiwa vile na Suarez
Suarez alionekana akimng`ata Ivanovic
Ivanovic
ameliambia gazeti la Serbia, Vecernje Novosti kuwa wakati tukio lile
likitokea alishangaa sana na kushituka, lakini baada ya mechi kumalizika
alitulia na kusahau kilichotoke.
Ivanovic alisema “siku ya kesho yake tuliongea kwa simu na nilikubali msamaha wake, sikumfokea kwa kitedo kile pia sikumtetea”.
Aliendelea kusisitiza kuwa “Kwangu mimi nimemsamehe bure, inaweza kutokea lakini sijali sana”
Ivanovic (kushoto) alipokuwa aamuonesha mwamuzi wa mchezo Kevin baada ya kung`atwa na Luis Suarez
Ivanovic amesema amekubali kumsamehe Luis Suarez
0 comments:
Post a Comment