Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) limempongeza bondia maarufu wa kitanzania
Francis Cheka kwa juhudi zake za kuwa bondia mzuri mwenye viwango vya
kimataifa katika uzito wa Super Middleweight.
Francis
Cheka aliweza kutetea mkanda wake wa IBF Africa uzito wa Super Middle
baada ya kumshinda kwa KO bondia Thomas Mashali aka “Simba asiyefugika”
tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.
IBF
inachukua fursa ya kumpongeza Francis Cheka baada ya ushindi huo ambao
umedhihirisha kuwa yeye kweli ni bingwa wa bara la Afrika. Francis Cheka
atarudiana na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiotcha mwezi wa Agusti
katika mpambano la kutetea mkanda wake.
Mpambano
wao wa marudiano utafanyika katika jiji la Blantyre nchini Malawi na
tayari majadiliano ya mpambano huo yanaendelea vizuri. Kampuni ya
“Mawenzi Boxing Promotion” ya nchini Malawi chini ya bwana Stephen
Mawezni ndiyoitakayoandaa mpambano huo.
Pambano
hili linakuja baada ya wadau kadhaa wa ngumi kuomba mabondia hao
warudiane walipoonyesha ujuzi mkubwa na ushindani katika mpambano wao
Desemba 26 mwaka jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeidi jijini Arusha
siku ya Boxing Day.
Baada
ya mpambano huo, IBF itampatia Francis Cheka nafasi ya kugombea mkanda
wa IBF wa Kimataifa (IBF International Super Middleweight) na mabondia
wa Ulaya au Marekani. Hii ni kudhihirisha kuwa Francis Cheka hana tena
mpinzanai nchini Tanzania na kumpambanisha na mabondia wa kitanzania ni
kumpotezea muda na uwezekano wake wa kutengeneza jina na pesa.
Wakati
huo huo bondia Thomas Mashali bado ni bingwa wa Afrika ya Mashariki na
Kati (ECAPBF) katika uzito wa Middle kwani mkanda wake haukuwa kati ya
mikanda iliyogombewa kwenye mpambano uliomalizika Mei mosi.
0 comments:
Post a Comment