Okwi (kushoto) alikuepo mechi ya msimu wa mwaka jana na safari hii hayupo, Simba bila yeye itaweza?
Na Baraka Mpenja
Kwa
wale wenye roho nyepesi watapata shida kubwa sana katika uwanja wa taifa
jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni ambapo
mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro atapuliza kipenga kuashiria kuanza
kwa pambano la kukata na shoka, kukata na mundu baina ya watani wa
jadi, wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa Kubwa” dhidi ya mabingwa wapya wa
ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans.
Langoni kwa Simba asilimia kubwa Juma Kaseja anaweza kuanza au Abeid Dhaira, yeyote atakayeanza lango la Simba litakuwa salama.
Kwa
Yanga Ally Mustapha “Bartez” kwa mara ya kwanza ataidakia Yanga katika
mechi ya watani wa jadi, ni kipa mwenye uwezo mkubwa na leo hii
atasimama langoni huku mpinzani wake mkubwa Kaseja naye akiwa kibaruani.
Kwa
upande wa Simba, walinzi Masoud Nasoro Chollo anaweza kuanza kulia,
kushoto Miraj Juma na katikati Musa Mudde na Shomary Kapombe. Katika
safu hii ya ulinzi mchezaji ambaye hajawahi kukumbana na presha ya
pambano la watani wa jadi ni Miraj Juma pekee, wengine wote wanauzoefu
mkubwa na wanaweza kusimama kidete, lakini huyu kinda anatulia sana na
huwa hababaishwi na mafaza.
Ukuta
huu ambao ni bora utakuwa unakabiliana na wachezaji wa Yanga kati ya
Said Bahanuz, Jerry Tegete, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza, ambao
yeyote anaweza kuanza katika mchezo wa leo. Itakuwa burudani kubwa
sana.
Kwa
beki ya Yanga Mbuyu Twite anaweza kuanza kulia, kushoto Oscra Samwel
Joshua au David Luhende, na ngome ya kati, injinia Kelvin Patrick Philip
Yondan na Nadir Haroub “Canavaro” watasimama.
Ukuta
huu utakumbana na presha kubwa kutoka kwa nyota wa simba ambao
watapangwa na kocha wao, inawezekana akaanza Amri Kiemba ambaye
hatabiriki atacheza wapi au Ramadhan Singano “Messi” .
Viungo
watachuano kufa mtu, kwa upande wa Mnyama, Musa Mude anayecheza chini
na mbele yake husimama Abdallah Seseme “Dullah” au Mwinyi kazimoto
Mwitula huku viungo wa pembeni wakisimama wachezaji wawili wenye kasi
kubwa sana Mrisho Khalfan Ngasa “Anko” na Haruna Chanongo.
Kwa Upande wa Yanga,Athman Idd “Chuji” atacheza chini, juu yake Domayo, kulia Simon Msuva na kushoto Haruna Hakizima Niyonzima.
Wachezaji wote hao wamekamilika sana na wana uwezo mkubwa wa kucheza soka, na leo hii itakuwa raha kubwa sana uwanja wa taifa.
Watu
wengi wanaipa Yanga nafasi ya kushinda kwa madai kuwa inawatumia
wachezaji wote wenye uzoezfu na mechi ya watani wa jadi, wakati Simba
inawatumia vijana wao waliowapandisha kutoka timu B.
Hakuna
ukweli, Mnyama kikosi chake kimechanganya damu na kina wachezaji vijana
walioaminiwa na kocha Mfaransa Patrick Liewig kutokana na uwezo wao wa
kucheza soka.
Timu
yoyote inaweza kuibuka na ushindi, endapo Yanga watawadharau Simba kwa
kutumia vijana wao, watakwenda na maji na pengine kutibuliwa sherehe zao
za kukabidhiwa kombe.
Kwa
upande wa Simba walishapoteza ubingwa na wanahitaji heshima mbele ya
watani wao wa jadi, hivyo wamejiandaa kwa uzuri sana kupambana na Yanga
yenye wachezaji wazuri sehemu zote na wamekaa pamoja kwa muda mrefu,
walienda hadi Uturuki, si mchezo kwa kweli.
Nao
Simba walienda Oman ingawa ziara yao haijawanufaisha sana, lakini bado
si haba, kikosi wanacho na wanaweza kupata ushindi leo kama wataamka
vizuri.
Kila
upande umejigamba sana kwa takribani wiki moja ya maandalizi, hatimaye
saa zazidi kuyoyoma na leo hii saa 10 kamili kipute kinaanza uwanja wa
taifa.
Mwenye
macho haambiwi Tazama, kama uko njema mfukoni, jiandae kwenda uwanja wa
taifa, na mechi hiyo itatumiwa kugawa zawadi kwa washindi, hivyo
kutakuwepo na hafla fupi ya zoezi hilo.
Bingwa
ni Yanga, nafasi ya pili ni Azam fc ambao leo hii watakuwa Arusha, na
nafasi ya tatu wapo Simba, kama ilivyokuwa kwa Yanga msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment