Siku ya mechi ya watani wa jadi mashabiki wa Yanga walimbeba Ngassa na kumvulaisha jezi ya Yanga
Na Baraka Mpenja
Siku mbili
baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu soka ya Vodacom Tanzania
Bara, pilikapilika za usajili zimeanza na mabingwa wa ligi hiyo,
Wanajangwani Dar Young Africans wameanza kwa kasi kubwa baada ya
kumsainisha mkataba wa miaka miwili nyota wa Simba mwenye kasi zaidi
Mrisho Khalfan Ngassa “Anko”.
Ngasa
alikuwa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Simba SC akitokea kwa wana
Lamba Lamba Azam FC na leo hii ametambulishwa rasmi mitaa ya Jangwani na
Twiga kuichezea klabu yake hiyo ya zamani tangu aondoke miaka mitatu
iliyopita.
Wakati
Ngassa akiwa anarejea Jangwani, habari zaidi zinasema kwamba Simba SC
nayo imepanga kujibu mapigo kwa kumsajili kiungo wa Yanga, Haruna
Hakizimana Fadhil Niyonzima kwa dau la Sh. Milioni 70 walizokubaliana
kwa mkataba wa miaka miwili.
Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameimbia MATUKIO DUNIAN kuwa klabu yao imeamua kumnasa Ngassa ili kuimarisha safu ya ulinzi ambayo imekosa mchezaji mshambuliaji wa kasi.
Mwalusako
amesema nyota huyo bado yuko katika kiwango kizuri na atawasaidia sana
wakati huu wa kampeni za kucheza ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
“Safu ya
ushambuliaji ni Simon Msuva pekee mwenye kasi zaidi, kwa sasa wakiungana
na Ngassa hakika tutafanya vizuri sana”. Alisema Mwalusako.
Kuhusiana
na taarifa za kumsajili Kapombe, Mwalusako amesema hawajazungumza kitu
kwa sasa, lakini kama inawezekana wanaweza kumsajili.
Pia
aliongeza kuwa sasa furaha ya mashabiki itakuwa kubwa kwani waliwaonesha
dalili za kumhitaji Ngassa tangu siku ya mechi ya watani wa jadi mara
baada ya kumvalisha jezi ya Yanga na kuonesha mabango ya kumtaka arudi
jangwani.
“Tumefanikisha nia yetu, tumefurahi sana, naamini sasa Yanga inazidi kuwa tishio”. Alisema Mwalusako.
Mtandao
huu umemtafuta mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Keptein
Zacharia Hans Poppe ili kupata ufafanuzi kuhusiana na taarifa hiyo.
Poppe
alisema wao hawana taarifa hiyo na wanashangaa kwa mchezaji huyo kusaini
mkataba na Yanga wakati tayari ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja
kuichezea Simba msimu ujao.
“Mimi
sijuia bwana, mkataba tulipeleka TFF na kama Yanga wamemsainisha leo
lazima wataupeleka TFF, sasa wenye maamuzi watabaki kuwa shirikisho”.
Alisema Poppe.
Poppe aliongeza kuwa Yanga wamekuwa maarufu wa kutokufuata taratibu za usajili kwasababu hawajawaona Simba na kuongea chochote.
“Wangekuwa
na busara wangekuja kuongea na sisi, lakini wanajifanyia tu mambo,
kiukweli Ngassa bado ni mchezaji wetu”. Alisema Poppe.
Ngassa aliichezea Simba SC mechi ya 27 na ya mwisho Jumamosi
katika kipindi cha kuwa kazini Msimbazi, wakati ilala mabao 2-0 mbele ya
Yanga. Katika mechi 27 alizoichezea Simba SC, zikiwemo za Ligi ya
Mabingwa mbili, kirafiki kadhaa na Ligi Kuu, Ngassa amefunga jumla ya
mabao saba na kutoa pasi za mabao 13.
Baada ya mechi dhidi ya Yanga Jumamosi, mashabiki wa timu ya Jangwani walimfuata Ngassa na kumvalisha jezi ya timu hiyo, jambo ambalo lilichafua hali ya hewa kwa mashabiki wa Simba.
Ngassa
alisajiliwa Azam Mei 21, mwaka 2010, kwa dola za Kimarekani 40,000,
zaidi ya Sh. Milioni 60 kutoka Yanga SC, huku yeye mwenyewe akipewa dola
30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45.
Alitua Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar ya Bukoba, ambayo ilimtoa Toto African ya Mwanza.
Alitua Yanga kwa mara ya kwanza mwaka 2006, akitokea Kagera Sugar ya Bukoba, ambayo ilimtoa Toto African ya Mwanza.
0 comments:
Post a Comment