Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Safari
ya Jose Mourinho kurejea Chelsea inaweza kutokamilika na hatimaye
kujiunga na Manchester United kumrithi kibabu Alex Ferguson ambaye sasa
safari yake imefikia ukingoni baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 27
na kutwaa mataji 49.
Hali
hiyo imejitokeza baada ya mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich
kushindwa kulipa fidia kwa klabu ya Real Madrid kutokana na kuvunja
mkataba wa Mourinho na klabu hiyo.
Mwaka
2006 Abramovich alimlipa Mourinho Pauni milioni 18 baada ya kumfukuza
na sasa anatakiwa kulipa fidia ya Pauni milioni 20 kama ada ya
kumhamisha kocha huyo kurejea darajani

Jose Mourinho kurejea Chelsea yapo mawili, kweli au hapana baada ya mmiliki wa klabu hiyo kushindwa kulipa fidia

Kocha huyo ndiye chagua namba moja la kumrithi kocha wa muda wa Chelsea Rafa Benitez, lakini Chelsea wanahitaji kuboresha zaidi kikosi chao zaidi ya mwaka 2004 ambapo Mourinho alijiunga kabla ya kufukuzwa 2006 akitokea klabu ya FC Porto ya Ureno.
Mourinho
kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kumrithi Ferguson lakini kwa sasa kocha
wa Everton David Moyes anaonekana kupewa nafasi kubwa zaidi


Rafa Benitez jana alifunguka kuwa dunia nzima inajua kuwa Mourinho anataka kurudi tena darajani.
Benitez
Alisema ” Unajua kila mtu anajua kuwa msimu ujao Chelsea itakuwa na
kocha mpya na hiyo inajulikana wazi, kila mtu anajua nani anakuja sasa.
Mimi naangalia zaidi kazi yangu ya sasa na si kuangalia ya mbele”.

Chelsea wanahitaji kumdhibiti zaidi Mourinho baada ya kurejea kuliko mwaka 2004 hapo juu
0 comments:
Post a Comment