Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge akizungumza na waalikwa
kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa habari Duniani
iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi utakao kuwa
ukisaidia waandishi wa habari pindi wapatapo matatizo wakiwa kazini.
Kushoto ni Mzee Kassim Mapili wa Mjomba waliosherehesha usiku huo kwa
buradani ya aina yake.(Picha na Dewji Blog).
Baadhi
ya Wanahabari walioshiriki kwenye Gala Dinner ya siku ya Uhuru wa
Habari iliyoenda sambamba na Uzinduzi wa Mfuko wa Mwangosi kusaidia
waandishi wa habari ambao wamepata matatizo wakiwa kazini.
Blogger
Pamela Mollel (katikati) wa Jamii Blog ya jijini Arusha akibadilishana
wanahabari wenzake Tonia Kasoni( kushoto) wa Radio 5 pamoja na Mhariri
wa Sibuka TV wakati wa hafla hiyo.
Mjane
wa Marehemu Daudi Mwangosi na mtoto wa mwisho wa marehemu wakati wa
uzinduzi wa Mwangosi Fund utakaokuwa ukisaidia waandishi wa habari
wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya
Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta
habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6
siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi wa Tuzo hizo atajinyakulia
Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
Mzee
Kassim Mapili wa Mjomba Band akikung’uta gitaa wakati akipiga wimbo wa
Mbaraka Mwishe” Njoo mjionee Morogoro”….wakati wa hafla ya kuchangisha
fedha za mfuko wa Daudi Mwangosi zilizoenda sambamba na uzinduzi wa
mfuko huo katika hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mmoja
wa waandishi wa siku nyingi kwenye tasnia ya habari ambaye pia ni
Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanawake Bi. Leila Sheikh akiimba
nyimbo za zamani pamoja na Mjomba Band inayoongozwa na Mzee Kassim
Mapili na Mrisho Mpoto.
Bi.
Leila Sheikh akisakata Rhumba la enzi hizo sambamba na Mzee Makwaiya
Wakuhenga wakati Gala Dinner katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari
Duniani kwenye Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa kuamkia leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan.
Wanahabari kutoka Zanzibar nao walijumika na wenzao wa Bara kutoka nchini za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Gala Dinner.
Wakongwe katika tasnia ya habari hapa nchini akiwemo Mzee Salim Salim na Mzee Hamza Kasongo na wenzao wakibadilishana mawazo.
Mgeni
rasmi kwenye Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari duniani
ulioenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu kilichoandaliwa na Media
Council Tanzania (MCT) pamoja na Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya Habari
Kusini mwa Jangwa la Afrika Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw.
Assah Mwambene akitoa salamu za Rais Kikwete za Pongezi kwa wanahabari
Tanzania kwa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambapo Serikali
imeahidi kushirikiana na wanahabari bega kwa bega kwa mustakabali wa
kuboresha tasnia hiyo.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene
akizindua Ripoti ya Habari hapa nchini ya mwaka 2012 iliyoandaliwa na
Media Council of Tanzania (MCT) aliyeshika kitabu hicho ni Afisa Mipango
Mwandamizi wa Taasisi ya Media Council of Tanzania (MCT) Bi. Alakok
Mayombo na Mjumbe wa MCT Bw. Allan Lawa na MC wa Gala Dinner hiyo Makamu
Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane
Mihanji.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene,
Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera na mwakilishi wa
Ubalozi wa Ireland kwa pamoja wakizuindua Kitabu cha Uhuru wa Vyombo vya
Habari Kusini mwa Jangwa la Afrika kilichandaliwa na MISA katika Gala
Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene akionyesha kitabu “SO
THIS IS DEMOCRACY” mara baada ya kukizindua rasmi.
Usia Nkhoma wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na mwanahabari mwenzake wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo.
Mzee
Hamza Kasongo akiendesha Harambee kwa wanahabari na wahariri kwa ajili
ya kuchangisha mfuko wa Mwangosi utakaokuwa ukisaidia wanahabari pindi
wapatapo matatizo kazini.
Stella Vuzo wa UNIC akitangaza ahadi yake binafsi ambapo ameahidi kutoa Dola 300 kuchangia Mfuko wa Mwangosi.
Mwenyekiti
wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera akitoa ahadi yake binafsi ambapo
ameahidi kuchangia Laki moja huku Misa-Tan imetoa ahadi ya Shilingi
Milioni moja kuchangia mfuko wa Mwangosi uliozinduliwa rasmi usiku wa
kuamkia leo katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha.
Mwakilishi kutoka BBC ambao nao pia waliguswa na kuchangia mfuko wa Mwangosi kiasi cha Shilingi Milioni Mbili.
Mwendeshaji
wa Harambee hiyo Mzee Hamza Kasongo akitangaza kiasi cha fedha
zilizokusanywa kwenye Harambee hiyo ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni
19 wakati wa Gala Dinner ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari
duniani.
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene
akikabidhi fedha taslim shilingi laki 5 zilizokusanywa kwenye Harambee
hiyo kwa Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
Bw. Kenneth Simbaya.
0 comments:
Post a Comment