Mahojiano na Domayo yamefanywa na mmiliki wa blog hii, Baraka Mpenja na mwandishi wa mtandao wa Fullshangwe
Beki
wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (kushoto) akiwa na Frank Domayo na
Simon Msuva wakati waki katika kambi ya Yanga nchini Uturuki.
Mipango
ua kunyakua ubingwa ilianza baada ya kumalizika ka mzunguko wa kwanza
ambapo Yanga walienda kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki na
kurejea nchini kwa ahadi ya kutokupoteza mchezo hata mmoja. Domayo
amesema hapo ndipo walipoanza kujiweka sawa na mafanikio kuonekana jana
uwanja wa taifa
Sherehe za kushangilia taji la ligi kuu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam huku wakiwa wamewaadhibi Simba mabao 2-0
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
FULLSHANGWE: Hello! Frank Domayo!, Pole na uchovu wa mechi ya jana.
DOMAYO:
Daah! Tumeshapoa anko, niambie Baraka? mimi nipo kaka, unafikiri Kuna
cha kufanya basi! tunafurahia ubingwa wetu tu, napumzika tu hapa nilipo
baada ya shughuli nzito ya jana.
FULLSHANGWE: Vipi Domayo baada ya kupangwa katika kikosi cha kwanza hapo jana na kuanza mechi ulikuwa unawaza nini?
DOMAYO:
Eeeh! wee acha tu! nilikuwa nawaza jinsi ya kuisaidia timu yangu
kushinda mchezo wa watani wa jadi, kama ulibyoona umati mkubwa kama ule.
Haikuwa kazi rahisi kwangu.
FULLSHANGWE: Uliogopa mashabiki?
DOMAYO:Hapana, mimi nilichukulia Changamoto tu, nilikuwa sawa kwa lolote tu.
FULLSHANGWE: Baada ya kushinda mchezo wa jana dhidi ya Simba na kukabidhiwa Kombe umejisikiaje Domayo?
DOMAYO:
kiukweli! Binafsi nimefurahi sana kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi kuu
soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013 nikiwa na klabu kubwa ya Dar
Young Africans.
FULLSHANGWE: Jana ulikuwepo katika kikosi cha kwanza cha Yanga, ulijisikiaje?
DOMAYO:
Nilijisikaia furaha ikizingatiwa mechi ya jana ilikuwa ya mwisho na
inatukutanisha na watani wetu wa jadi. Nilikuwa na furaha kutajwa kikosi
cha kwanza ambacho kilikuwa na malengo ya kuongeza furaha zaidi ya
kutwaa ubingwa msimu huu, nilijua raha itakuwa kubwa zaidi tukiwafunga
Simba na imetokea hivyo.
FULLSHANGWE: Je, uliwahi kuwaza kuwa ipo siku utatwaa ubingwa na umri mdogo kiasi hicho?
DOMAYO:
Yaah! Siku zote ilikuwa ndoto Yangu kuwa ipo siku nitatwaa ubingwa
katika umri wangu mdogo na imetokea hivyo, daah! nimefurahi sana, hata
ndugu, jamaa na marafiki zangu wamefurahi sana na kunipongeza.
FULLSHANGWE: Ubingwa wa msimu huu unajenga picha gani kwako?
DOMAYO:
Kaka unanipa somo kubwa sana, Unajua lazima ujue kitu kimoja kuwa kila
mchezaji anapenda kutwaa vikombe, ubingwa wa msimu huu unanijengea picha
ya kujipanga zaidi na kuitumikia klabu yangu kwa nidhamu kubwa ili kama
namaliza umri wangu wa soka ije kubaki historia kwangu na kwa wanangu,
au vipi bwana!!
FULLSHANGWE: Unamzungumziaje kocha Ernie Barandts aliyekupa nafasi muda wote?
DOMAYO:
Ni Kocha mzuri sana, anapenda sana wachezaji wazingatie nidhamu ya
mazoezi na maelekezo yake, mara zote nimekuwa nikifanya kama kocha
anavyotaka na ndio maana nimekuwepo katika kikosi cha kwanza kwa muda
wote, najisikia furaha sana, kizuri chajiuza bwana! Nitakaza hivi hivi!
FULLSHANGWE: Msimu umeisha, utabaki kuwa Yanga au utaihama?
DOMAYO:
Mimi ni mchezaji wa Yanga na nitabaki kuwa mchezaji wa Yanga, binafsi
najipanga vizuri kuyakabili mashindano ya kimataifa ambayo
yatanikutanisha na wachezaji wa mataifa mbambali barani Afrika.
FULLSHANGWE: Wenzenu Simba mwaka huu wamekalia kuti la moto, mwaka ujao kazi kwenu, unaonaje?
DOMAYO:
Tumeshinda ubingwa, lakini daah! Kazi ipo, bado tuna changamoto ya
kucheza ligi ya mabingwa, kama mnavyojua kule kuna timu nzuri na
wachezaji wazuri, usiwe na wasiwasi tutajipanga tu.
FULLSHANGE: Umeionaje ligi kuu msimu huu?
DOMAYO:
Ligi ya mwaka huu ilikuwa na changamoto kubwa kutoka kwa timu shiriki
hadi kwa mashabiki wa timu ambao siku zote wanahitaji ushindi. Mara
nyingi mashabiki wa timu kubwa wanapenda ushindi, mchezaji ukikosea
wanachukia, mimi hainipi shida, nachukulia changamoto tu kwani hata
ulaya mashabiki ndio wanaochangamsha soka.
FULLSHANGWE: Umeitwa na kocha Kim Paulsen katika kikosi cha Taifa stars, unajisikiaje?
DOMAYO:
Najisikia furaha! Nimefurahi sana! Unajua kuna vijana wengi wenye
uwezo, lakini kocha amekuwa ikinipa nafasi ya kucheza zaidi. Mwalimu ana
falasafa yake, kuna wachezaji wengi wanaofaa, lakini kanichagua mimi.
Binafasi sitamuangusha hata kidogo.
FULLSHANGWE: Vipi una ndoto za kucheza soka la kimataifa?
DOMAYO:
Una uliza ndizi Tukuyu! Naota sana kaka, natamani kucheza soka la
kulipwa kama wanavyofanya waliotutangulia, nadhani siku itafika na
nitapata nafasi, nazingatia sana nidhamu ya soka.
FULLSHANGWE: Asante sana Frank Domayo kwa ushirikiano wako, kila la heri na hongera sana kwa ubingwa?
FULLSHANGWE: Shukurani sana Anko! Karibu sana na kazi njema kwako, naipenda Fullshangwe.
0 comments:
Post a Comment