Na Baraka Mpenja Kwa Msaada wa Sportsmail.com
MKONGWE
anaekaribia Miaka 40, Kevin Phillips, leo amewapandisha Daraja Crystal
Palace baada yakufunga Penati katika Dakika ya 105 baada Mchezaji Nyota
wa Fainali hii, Wilfried Zaha, Chipukizi wa Manchester United, kuchezewa
faulo katika Fainali ya Mechi za Mchujo ya kupandisha Timu moja
iliyochezwa Uwanja wa Wembley na Crystal Palace kuifunga Watford Bao
1-0.
Crystal
Palace inaungana na Timu zilizopanda moja kwa moja Mabingwa wa Daraja
la Championship, Cardiff City, na Timu iliyomaliza Nafasi ya Pili, Hull
City, kupanda Daraja na kucheza BPL, Barclays Premier League, Msimu ujao
wa 2013/14 utakaoanza Agosti 17.
Hadi
Dakika 90, ambazo Crystal Palace walionekana bora huku Wilfried Zaha
akitamba, Bao zilikuwa 0-0 na Dakika za Nyongeza 30 zikaongezwa.
Katika
Dakika ya mwisho ya Kipindi cha Kwanza cha Dakika 15 mwanzo za Nyongeza
30, Zaha alipokuwa akichanja mbuga ndani ya Boksi Beki wa Watford,
Marco Cassetti, alimkata na Refa Martin Atkinson hakusita kuashiria
Penati.
Penati
hiyo, licha ya Kipa wa Watford, Manuel Almunia, Kipa wa zamani wa
Arsenal, kuifuata, ilipigwa na kufungwa kifundi na Mkongwe Kevin
Phillips ambae aliingizwa toka Benchi kwenye Kipindi cha Pili cha Dakika
90 za mwanzo.
Crystal Palace
-Crystal
Palace wamerudi tena BPL kwa mara ya 5, ikiwa ni Rekodi, baada ya
kupanda Daraja mara 4 hapo nyuma lakini mara zote walidumu Msimu mmoja
tu kwenye BPL katika Misimu ya 1992/93, 1994/95, 1997/98 na 2004/05.
Akiongea
mara baada ya Mechi hii, Wilfried Zaha, Miaka 20, ambae ndie aliteuliwa
Nyota wa Mchezo huu, alisema: “Nimechoka na sina hata cha kusema! Ni
ndoto iliyotimia! Hiki ndicho nilichotaka, kuiacha Palace nikijua
wanatinga Ligi Kuu!”
Zaha
alianza kuichezea Crystal Palace tangu ana Miaka 10 tu na Januari Mwaka
huu, Sir Alex Ferguson, Meneja wa Manchester United anaestaafu,
alimnunua ili achezee Old Trafford lakini akabakishwa Crystal Palace kwa
Mkopo hadi Msimu huu unapomalizika na sasa amemaliza kwa furaha kwa
kuipandisha Daraja.
Super Eagles: Crystal Palace wamerudi tena ligi kuu soka nchini England baada ya kuikosa kwa miaka saba
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Moxey, Zaha, Jedinak, Garvan, Dikgacoi, Williams, Wilbraham
Akiba: Price, Richards, Bolasie, Phillips, O’Keefe, Ramage, Moritz.
Watford: Almunia, Doyley, Ekstrand, Cassetti, Anya, Chalobah, Hogg, Pudil, Abdi, Deeney, Vydra
Wilfried Zaha aliifungia bao timu yake kwa mkwaju wa penato baada ya kufanyiwa madhambi na Marco Cassetti
ZAWADI KUBWA: Mkongwe Kevin Phillips amefunga bao la ushindi na kuirudisha ligi kuu Engalnd
NTOTA YAKE JAMANI: Zaha amecheza kwa kiwango kikubwa sana na kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo
MTU
MAALUMU: Kocha anayeondoka Real Madrid, Mreno mwenye maneno mengi Jose
Mourinho alihudhuria mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa taifa wa Wembley
SHANGWE KUBWA: Mashabiki wa Crystal Palace wakishangilia katika uwanja wa Wembley
Mashabiki wa Watford wakishangilia timu yao kabla ya kuanza kwa kipute hicho
0 comments:
Post a Comment