Na Frank Mvungi na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI
ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya Umoja wa nchi za
Ulaya( EU) utakaowezesha Tanzania kupatiwa shilingi bilioni 20 kusaidia
maendeleo katika sekta ya kilimo cha miwa kwa wakulima wa Visiwa vya
Zanzibar.
Mkataba
huo ulisainiwa jana jijini Dar es salaam kati ya Waziri wa Fedha na
Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi,
ambapo unategemewa kuisaidia serikali katika kuondoa umasikini kwa
wananchi wake na kuiwezesha nchi kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta
ya kilimo.
Waziri
Mgimwa alisema kuwa msaada huo pia utasaidia kuwajengea wananchi uwezo
wa kutekeleza kilimo chenye tija na kupanua soko la bidhaa zitokanazo
na miwa kwani miundo mbinu ya maeneo ya Uzalishaji pia itaboreshwa
katika utekelezaji wa mradi huo.
“Kwa
niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania napenda
kuishukuru jumuiya ya umoja wa nchi za Ulaya kwa juhudi kubwa
wanazochukua kusaidia maendeleo ya nchi yetu, asanteni sana,” alisema
Waziri Dk.Mgimwa.
Naye
balozi wa EU, Mhe. Filberto Sebrigondi alisema wameridhishwa na
mikakati ya serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ndio maana
wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kusaidia wananchi
kufikia maendeleo ya kweli hivyo wameamua kusaidia sekta ya miwa ili
iweze kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
Pia
balozi Sebrigondi alisema kuwa wataendelea kusaidia bajeti ya Serikali
ya Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwa Tanzania
imeonyesha nia ya dhati katika kukuza uchumi wake na kuweka mazingira
mazuri kwa wananchi wake ili waongeze tija katika uzalishaji.
Alisema
katika kipindi kilichopita asilimia 87% ya fedha lizizotolewa kwa
Serikali ya Tanzania zimeshatumika katika miradi ya maendeleo, hivyo
ameahidi kuwasaidia wanachi wanaojihusisha na kilimo cha miwa ili
kuwajengea uwezo, kufanya tafiti na kutoa elimu ya utunzaji mazingira
katika maeneo yatakayonufaika na msaada huo.
Umoja
wa nchi za Jumuiya ya Ulaya umekuwa kwa muda mrefu ukisaidia sekta
mbalimbali za maendeleo hapa nchini ikiwa ni moja ya washirika wa
maendeleo wa Tanzania ambapo baadhi ya Sekta zinazonufaika ni sekta ya
kilimo cha Kahawa, na Miwa, sekta ya Barabara, Elimu, nishati ya Umeme
ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment