Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas
Kassongo (kushoto), akimkabidhi Meneja wa timu ya Friends Rangers,
Shaaban Marsila Sh 500, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia
timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu. Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas
Kassongo (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu
Sh 700, 000 ikiwa ni mchango wa chama hicho kusaidia timu hiyo katika
Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu
CHAMA
Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimezizawadia timu
tatu za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zilizofanikiwa kucheza
Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Mei 12 mwaka huu.
Makabidhiano
hayo yalifanyika jana Alhmaisi (Mei 9) jioni kwenye ofisi za chama
hicho, zilizopo makutano ya mtaa wa Mafia na Bonde, ambapo Red Coast
waliokuwa washindi wa kwanza walikabidhiwa Sh laki saba ( 700, 000/=),
huku Abajalo wao wakizawadiwa Sh laki sita (600, 000/=) na Friends
Rangers wakijipatia Sh laki tano (500, 000/=).
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, lengo la timu hizo
kukabidhiwa fedha hizo ni kuzihamasisha ili ziweze kujiandaa na hatimaye
kufuzu kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Mwenyekiti
wa DRFA, Almas Kassongo, ndiye alikabidhi fedha hizo kwa wawakilishi wa
timu hizo huku akisema licha ya kiasi hicho cha fedha kuwa kidogo,
lakini itakuwa chachu ya kupata mafanikio.
Viongozi
waliohudhuria makabidhiano hayo kutoka DRFA ni Mkurugenzi wa Ufundi,
Joseph Kanakamfumo, Afisa Tawala, Said Pambalelo, Mjumbe wa Kamati ya
Ufundi na Mashindano, Daudi Kanuti na Mweka Hazina Ally Hassani.
Wawakilishi
wa timu ni Mwenyekiti wa Red Coast, Jumanne Ayubu, Meneja wa Friends
Rangers, Shaaban Marsila na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Abajalo,
Abbasi Ngau.
Wakati
huo huo, kamati ya ufundi ya DRFA kesho Jumamosi Harbours Club
Kurasini, itakutana na Viongozi wa soka la Wanawake (TWFA), Viongozi wa
soka la Vijana na Kamati ya Waamuzi ili kupanga utaratibu wa ligi na pia
kuandaa kozi ya makocha.
0 comments:
Post a Comment