Na Baraka Mpenja wa kwa msaada wa Sportsmail.com
Mlinda
mlango namba moja kwa sasa wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Diego
Lopez amesema klabu hiyo kumpoteza kocha mwenye ubora wa hali ya Juu,
Mreno Jose Mourinho ni hasara kubwa sana, huku akisisitiza kuwa baadhi
ya wachezaji wa timu hiyo nao wamejisikia vibaya.
Mourinho
amebakisha mechi moja kuingoza Real Madrid huku kocha wa zamani wa
Chelsea ambaye amewapa ubingwa PSG katika ligi ya Ufaransa msimu huu
Carlo Anceloti akitajwa kurithi mikoba yake, wakati huo Mourinho
akitajwa kurudi Chelsea kurithi mikoba ya Rafa Benitez aliyekuwa kocha
wa muda wa klabu hiyo.
Mourinho
amekaa misimu mitatu nchini Hispania, lakini msimu wa mwaka huu umekuwa
mbaya kwake baada ya kushindwa kutwaa kikombe hata kimoja huku rais wa
klabu hiyo Florentino Perez akithibitha kuwa msimu huu ni wa mwisho kwa
kcoha huyo mwenye ngebe nyingi zaidi.
Lopez
aliyefaidika sana kwa kupata namba katika kikosi cha kwanza baada ya
Mourinho kukosa uelewano mzuri na kipa na nahodha wa klabu hiyo Iker
Casillas aliongeza kuwa Mourinho ni kocha mwenye haki siku zote.
“Itakuwa
hasara kubwa kwa Madrid, Mourinho ni kocha mzuri sana, kwa upande wangu
amenifanyia mambo makubwa na kunifanya nijiamini zaidi nikikaa
langoni”. Alisema Lopez.
ANARUDI ZAKE MJINI: Jose Mourinho alikuwepo Wembley kutazama mechi ya Watford dhidi ya Crystal Palace
DILI HILO!!: Mourinho anatarajiwa kuichukua Chelsea iiliyomalizana na kocha wa muda Rafa Benitez
MBAYA MNO!!: Diego Lopez akijilaumu baada ya Real Madrid kutoa sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Real Sociedad jana
0 comments:
Post a Comment