
Nahodha wazamani wa timu ya taifa ya
Soka ya Uingereza David Beckham ameamua kustaafu mwisho wa msimu huu.
Beckham mwenye umri wa miaka 38 alijiunga na
timu ya Paris St-Germain mapema mwezi wa Januari kwa kandarasi ya miezi mitano.
Wakati wa kutia saini kandarasi hiyo mwamba
huyo wa Uingereza alitangaza kwamba mshahara wake wote atautoa kwa mashirika ya
kutoa msaada.
Beckham alijunga na timu ya Manchester United
akiwa na umri wa miaka 14 na kufaulu kuichezea klabu hiyo mara 398 huku
akishinda makumbe sita ya Ligi kuu na kombe la klabu bingwa bara Ulaya.
"Naishukuru sana timu ya PSG kwa kunipa
fursa ya kuendelea kucheza lakini nahisi kuwa huu ni wakati mzuri kwangu
kumaliza kazi yangu ya kucheza mpira " amesema.
Pamoja na PSG kubeba kombe la Ligue 1 la
Ufaransa , katika uchezaji wake Beckham amezoa jumla makombe 19 - 10 kati yao
yakiwa ni makombe ya ligi kuu mbali mbali.
Bechkam ndie mchezaji wa kwanza wa Uingereza
kuwahi kubeba makombe ya ubingwa wa Ulaya akichezea timu katika nchi nne
tofauti.
0 comments:
Post a Comment