Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Dili la kustaafu lazidi kuitikisa nchi ya Uingereza baada ya magwiji wa soka na kocha maarufu kustaafu kufundisha soka.
Wiki
moja baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, Paul Scholes, leo hii
mchezaji wa zamani wa Man United na nahodha wa zamani wa England DAVID
BECKHAM ametangaza kutundika daluga.
Beckham
mwenye umri wa mika 38, ameisadia Paris Saint-Germain PSG Kutwaa mwari
wa Ligue 1 nchini Ufaransa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 19 mwishoni
mwa wiki iliyopita
Pamoja na kupewa ofa ya
mkataba mpya na timu hiyo ya Ufaransa, mkongwe huyo atastaafu baada ya
mchezo wa mwisho tarehe 26 mwezi huu .
Alisema: “Shukrani sana kwa
PSG kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwa hapa lakini sasa nadhani ni muda
sahihi wa kustaafu, kucheza kwenye soka la kiwango cha juu”
Beckam alianza kucheza akiwa na Manchester United, akifunga mabao 85 katika mechi 394, kabla ya kuhamia Real Madrid.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer.
Aliondoka Spain kwa uhamisho mnono kujiunga na LA Galaxy mwaka 2007 pia aliwahi kucheza kwa mkopo mara kadhaa kwenye klabu ya AC Milan wakati akiwa kwenye Major League Soccer.
KWAHERI SOKA: David Beckham atatundika dalagu baada ya kucheza soka kwa muda mrefu
Beckham anastaafu soka akiwa tayari ameshamsaidia kocha wa PSG Carlo
Ancelotti ambapo nyota huyo alishangila ndoo hiyo na mwenzake Zlatan
Ibrahimovic (pichani kulia)
PUMZIKA SALAMA: Beckham huyo kuutazama mpira kupitia Runinga akiwa nyumbani mara tu atakapostaafu mwishoni mwa msimu huu.
HISTORIA YA MICHEZO ALIYOCHEZA BECKHAM NGAZI YA KLABU
Manchester United – mechi 394, alifunga mabao 85
Preston North End (kwa mkoo) – mechi 5 , alifunga mabao 2
Real Madrid – mechi 115, alifunga mabao 20
LA Galaxy – mechi 118 , alifunga mabao 20
AC Milan – mechi 33, alifunga mabao 2
PSG – mechi 11, hajafunga bao lolote
Preston North End (kwa mkoo) – mechi 5 , alifunga mabao 2
Real Madrid – mechi 115, alifunga mabao 20
LA Galaxy – mechi 118 , alifunga mabao 20
AC Milan – mechi 33, alifunga mabao 2
PSG – mechi 11, hajafunga bao lolote
0 comments:
Post a Comment