Kabla hatujaangazia kipute cha watani wa jadi, Simba na Yanga, MATUKIO DUNIANI ikujulishe matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa leo hii.
Toto
African tayari wameshashuka daraja licha ya kuibuka na ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya maafande wa Ruvu shooting kutoka mkoani Pwani katika dimba
la CCM kirumba Mwanza.
Mgambo
wamefanikiwa kubaki ligi kuu baada ya leo hii kuibuka na ushindi wa bao
1-0 dhidi ya Africa Lyon katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
JKT Ruvu chini ya kocha Keny Mwaisabula wameshinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Chamazi.
Wajela jela Tanzania Prisons wamefungwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine mkoani Mbeya.
JKT Oljoro wamefungwa bao moja kwa bila na Azam fc katika uwanja wa Sheik Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.
Matokeo
ya leo yanamaanisha, Africa Lyon, Toto Africans ya Mwanza na Polisi
Morogoro zimeporomoka daraja na kuzikaribisha timu za Mbeya City, Rhino
Rangers na wauza Mitumba wa Ashanti United.
Sasa
turejee katika kipute cha aina yake kilichopigwa jijini Dar es salaam
uwanja wa taifa baina ya watani wa jadi Simba na Yanga.
Mabingwa wa ligi kuu bara msimu huu, Dar Young Africans wameongeza furaha yao zaidi leo hii baada ya kuwaadhibu Simba mabao 2-0.
Mabao
ya Yanga yamefungwa na Didier Kavumbagu dakika ya tano ya kipindi cha
kwanza na msumari wa pili umefungwa na Hamis Kiiza “Diego” katika dakika
ya 63 akitumia makosa ya mabeki Cholo na Mude walioshindwa kuosha mpira
langoni mwao.
Mbali na ushindi huo, mechi hiyo pia imetumika kugawa zawadi kwa washindi wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara msimu huu.
Uwanjani
yametokeo matukio ya aina yake, moja ni Mwamuzi wa mchezo Martin Saanya
kutoka Morogoro kupata ajali ya uwanjani baada ya kugongwa na kipepsi
cha mchezaji na kupasuka sehemu ya jicho dakika za lala salama.
Pia
katika dakika ya 26 Musa Mude alikosa penati waliyozawadiwa na Saanya
baada ya Canavaro kumfanyia madhambi Mrisho Ngasa katika eneo la hatari.
Kipa Ally Mustapha “Bartez” alidaka shuti hafifu ama dhaifu alilopiga Musa Mude
Pia
Kituko kilitokea baada ya Canavaro kumzonga mwamuzi kama alivyofanya
msimu uliopita katikka mchezo dhidi ya Azama FC ambapo walifungiwa kwa
kumpiga mwamuzi Israel Nkongo.
Dakika
ya 85 kipindi cha pili, Nizar Halfani alipiga shuti kali na la mwaka
ambapo baada ya kugonga mwamba wa chini lilimgonga kipa Juma Kaseja
sehemu ya paji la Uso na kulala kwa muda wa dakika kadhaa.
Mchezaji
wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu akikokota mpira mbele ya mchezaji wa
timu ya Simba Abdallah Seseme katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , hivi
sasi ni kipindi cha pili na Yanga wanaongoza magoli 2 -0 dhidi ya Simba
ambayo imekosa penati katika kipindi cha kwanza wakati mchezaji wake
Mussa Mude akipiga vibaya mpira huo baada ya Mrisho Ngassa wa Simba
kuangushwa kenye eneo la hatari

Wachezaji wa timu ya Simba na Yanga wakiwania mpira wakati wa mchezo wao unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kupata goli la kwanza dhidi ya Simba.
Baada ya mechi kumalizika, makocha wa timu zote waliongea na waandishi wa habari.
Ernie
Brandts kocha wa Yanga alisema “ushindi huu ni wa timu yote,
niliwaambia wachezaji kabla ya mechi kuwa tunatakiwa kushinda kwa ajili
ya mashabiki na viongozi wetu, mafanikio haya ni kutokana na ushirikiano
mzuri tunaopewa na mwenyekiti wetu Manji na makamu bwana Sanga”.
Kocha
Simba Patrick Liewig alisema “ni sawa kupoteza mchezo, wamestahili
kushinda kutokana na mchezo mzuri, sina shaka, lakini wachezaji wangu
hasa sehemu ya ulinzi wamenighraimu sana, ukiangalia mabao yote
yamefungwa kutokana na uzembe”.
Wakati wa kugawa zawadi, kuna matukio ya aina yake ya kufurahisha na kuhuzunisha pia.
Kitebndo
cha wachezaji wa Simba kutokeo mbele ya mgeni rasmi wakiwa wamevalia
majinsi yao, malapa, na singalendi, hakika limeshangaza wengi na
ukizingatia mchezo huo ulikuwa unatazamwa na watu wengi zaidi duniani
kutokana na kurushwa na Supersport. kama ilikuwa sahihi kufanya vile,
unatakiwa kuangalia wenzetu wa majuu wakati wa kupokea zawadi
wanavaliaje.
Suala
la pili ni kitendo cha Jerryson Tegete kushangilia akiwa amebeba kombe
huku akivalia jezi nyekundu ya Simba aliyobadilishana na mmoja wa
wachezaji wa Simba.
Tukio
lingine ni kitendo cha Ngasa kubebwa na mshabiki wa Yanga huku akiwa
amevalishwa jezi ya Yanga wakati ni mchezaji wa Simba.
Haya ni baadhi ya matukio muhimu ambayo tumeyabaini katika mchezo huu.
0 comments:
Post a Comment