Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com, Soka In Bongo
JANA
Usiku huko New York, Marekani kwenye Uwanja wa Yankee, Manchester City
iliwatandika Chelsea Bao 5-3 katika Mechi yao ya pili ya Kirafiki huko
USA.
Juzi, wakicheza Mjini St Louis, Man City waliitandika Chelsea Bao 4-3 licha ya kutanguliwa Bao 3-0.
MAGOLI:Man
City 5-Barry Dakika ya 3, -Nasri 29 & 74, -Milner 55, -Dzeko 84,
kwa upande wa, Chelsea -Ramires Dakika ya 46 & 69, -Mata 82
Hii
ndio Mechi ya mwisho kabisa kwa Kocha wa Muda wa Chelsea, Rafael
Benitez, ambae alikuwa hapo Stamford Bridge kuanzia Novemba baada ya
Roberto Di Matteo kutimuliwa.
Katika
Mechi hii Chelsea walijikuta wako nyuma mapema tu katika Dakika ya 3 tu
baada ya makosa ya Kipa Hilario na Oscar na kumzawadia Gareth Barry
kufunga kilaini.
Hadi Mapumziko Chelsea walikuwa nyuma kwa Bao 2-0 baada Nasri kuifungia City Bao la Pili.
Kipindi
cha Pili kilianza kwa Ramires kuifungia Bao Chelsea na kufanya Mechi
iwe 2-1 lakini Milner akaipigia Bao City kwa shuti lililomshinda Kipa
Petr Cech alieingizwa badala ya Hilario.
Alikuwa
Ramires tena aliefunga Bao la Pili kwa Chelsea na gemu kuwa 3-2 lakini
Dakika 5 baadae Nasri akapiga Bao la 4 kwa City baada ya uzembe wa
Mabeki.
Frikiki
safi ya Juan Mata iliwafanya Chelsea wapate Bao la 3 na Mechi kuwa 4-3
lakini Dakika 2 tu baadae City wakafunga Bao lao la 5 kwa kigongo kikali
cha Edin Dzeko na kuifanya Mechi imalizike 5-3.
Fernando Torres anaamini kocha Rafa Benitez ameimarisha sana kikosi cha Chelsea katika muda wake
MOTO UNAWAKA: Torres (kulia) wa Chelsea alicheza jana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Man City nchini Marekani
Raha za ushindi nchini Marekani, si mchezo kwa kweli
Benitez
amewasaidia Chelsea kubeba kombe la ligi ya Uropa na sasa mkataba wake
amemalizika huku ikisemekana kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho
anaweza kurithi mikoba yake
VIKOSI:
Manchester City: Hart; Kompany (Nahodha), Zabaleta, Kolarov, Boyata; Nasri, Barry, Silvaa, Toure; Aguero, Tevez
Chelsea: Hilario; Luiz, Azpilicueta, Christensen, Ake; Ramires, Oscar, Obi Mikel, Loftus-Cheek; Ba, Torres (Nahodha)
0 comments:
Post a Comment