Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Siku
moja baada ya kutetea ubingwa wake wa IBF Afrika mbele ya mpinzani wake,
mtu wa watu Thomas Mashali “Simba asiyefugika” katika ukumbi wa PTA
usiku wa jana, bondia ambaye kwa sasa hana mpinzani nchini Tanzania,
mkazi wa mji kasoro bahari , Morogoro, Francis Cheka amesema siku zote
nidhamu kubwa ya kufuata maelekezo ya waalimu wake, kuzingatia mazoezi
na kutambua umuhimu wa kutunza afya yake ndii siri ya mafanikio yake
ulimwengu wa masumbwi
Cheka ameiambia MATUKIO DUNIANI
kuwa ushindi wa jana ni zawadi kwa wakazi wa Morogoro ambao siku zote
ni mashabiki wake wakubwa wakati wake huu wa maisha ya ndonga.
“Nilisema
toka awali kuwa nahitaji kushinda pambano hilo, mashabiki wangu
walinitaka kutetea ubingwa wangu, kwa kuzingatia maoni yao nilijipanga
kama kawaida yangu na kilichotokea jana nilijua tu”. Alisema Cheka.
Bondia
huyu mwenye ngumi kali kwa wapinzani wake aliongeza kuwa mabondia wa
Tanzania wana majina makubwa kwa vyombo vya habari na wana maneno mengi,
lakini yeye siku zote ni kuonesha vitendo tu
“Mie
sio msemaji sana ndugu yangu, unajua wengi wanasema sana wanapojiandaa
kukutana na mimi, lakini wanaangukia pua, Mashali alitamba sana na
akasema lazima amalize ufalme wangu wa sasa, nilitambua hilo nikamfanyia
mazoezi na hatimaye imefahamika”. Alisisitiza Cheka.
Cheka
alisema mpinzani wake ambaye ni bingwa mtetezi kwa ukanda wa Afrika
Mashariki na kati alicheza kwa kiwango kizuri tofauti na michezo yake
mingine, lakini kushindwa kwa “Nock Out” alistahili kutokana na uwezo
wake kuwa mdogo mbele yake.
“Cheka
atabaki kuwa cheka, amini usiamini mimi niko fiti sana, mashabiki wangu
wanajua hilo na ndio maana wanajenga imani kubwa na mimi”. Alisema
Cheka.
Baada
ya kuibuka na ushindi huo jana katika ukumbi wa PTA jijini hapa, Cheka
alizawadiwa gari aina ya Noah ambayo iliandaliwa rasmi na IBF Africa.
0 comments:
Post a Comment