Na Baraka Mpenja
Bingwa wa
IBF Afrika, bondia asiye na mpinzani kwa sasa nchini Tanzania , mwenye
makazi yake Mkoani Morogoro, Francis Cheka ameibuka na kudai kuwa mchezo
wa masumbwi haupewi kipaumbele na wadhamini wa michezo kama ilivyo kwa
soka.
Cheka akiwa mkoani Morogoro, mji kasoro bahari ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa serikali ya Tanzania na wadau wa michezo kwa ujumla wameutupa sana
mchezo wa ndonga ambao unafanya vizuri medani ya kimataifa.
“Unajua
mimi nashangaa sana, tukienda kushindana kimataifa huwa tunaimba wimbo
wa taifa kuashiria kuiwakilisha nchi, lakini hatupewi kitu na viongozi
wetu na tunabaki kuhangaika tu”. Alisema Cheka.
Cheka
aliongeza kuwa kwa sasa kila kampuni inakodoloa macho kudhamini kandanda
lakini hata kidogo hawajitokezi kudhamini masumbwi na kumwaga pesa
nzuri kwa mabondia ambao kila siku wanateseka na ukata katika maandalizi
yao.
Bondia
huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza masumbwi akiwa ulingoni alisisitiza
kuwa kila mchezo unahitaji mipango, fedha na uwezeshaji.
“Mimi
nawaeleza viongozi kitu kimoja, lazima wabadilike, natamani siku moja
nionane na Mheshimiwa Rais Dkt. Kikwete nimueleze jinsi tunavyohenyeka
katika mchezo huu ambao tukienda kimataifa tunaimba wimbo wa Taifa”.
Aliongea Cheka kwa hisia.
Cheka
alitolea mfano michuano ya Olmpic kuwa Taifa linawakilishwa na wabondia
wachache wakati serikali inaweza kusafirisha mabondi hata mia moja
kwenda kushiriki.
“Nia ya kuendeleleza masumbwi imekufa kabisa, cha msimgi lazima viongozi wetu wabadilike sana”. Alisisitiza Cheka.
Akizungumzia
suala la kuanzisha kituo cha kulea na kuibua vipaji vya mabondia
wachanga, Cheka alisema mpango huo upo lakini peke yake bado ni ndoto
kutokana na kukosa wadhamini.
“Mimi
Cheka nikisema najenga kituo cha kuchukua hata wanafunzi 50 ni uongo,
sina uwezo huo, lakini serikali inao uwezo wa kujenga kituo cha kuchukua
hata wanafunzi 1000 kwa mwaka, ila wamekosa nia tu”. Alisema Cheka.
Siku ya
mei mosi Cheka alitetea ubingwa wake wa IBF Africa na kutwaa zawadi ya
gari aina ya Noah baada ya kumtwanga Simba asiyefugika Thomas Mashali
katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.
Ushindi
huo ilimfanya Cheka kuendeleza ubabe kwa mabondia wa Tanzania na Afrika
baada ya kutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo.
0 comments:
Post a Comment