Na Eliphace Marwa – Maelezo
CHAMA
cha Wauguzi Tanzania kimesema kuwa vifo vya mama wajawazito pamoja na
watoto vimepungua sana nchini kutokana na kuboreshwa na kufikishwa kwa
huduma muhimu kwa walengwa.
Kauli
hiyo imetolewa na Rais wa chama hicho, Paulo Magesa wakati akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam juu ya Maadhimisho ya
Siku ya Waaguzi Duniani yatakayofanyika Mei 12 mwaka huu.
Magesa
alisema maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani
Rukwa, yatakuwa na kauli mbiu inayosema kuwa “Kuziba pengo kufikia
Malengo ya Milenia namba 6,5,4”.
Alisema
kuwa malengo hayo ya millennia yanalenga kuzuia vifo vya kinamama
wajawazito wakati wa kujifungua, kuzuia vifo vya watoto wenye umri chini
ya miaka mitano na kuzuia maambukizi ya Virusi Virusi UKimwi(VVU)
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“Pamoja
na changamoto nyingi tunazokutana nazo wauguzi bado tunajitahidi kwa
kadri ya uwezo wetu kuhakikisha na hii imeleta mafanikio makubwa
kwani”, alisema Magesa.
Alifafanua
kuwa pamoja na changamoto nyingi wanazokutana nazo wauguzi nchini,
bado wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma bora
zinawafikia walengwa na hilo limeleta mafanikio makubwa.
Katika
kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini chini ya
mpango wa Milenia,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imelenga kuhamasisha
akina mama kutumia njia salama za uzazi wa mpango na kuhakikisha
wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za mama na mtoto.
Katika
maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho kuanzia Mei 10 hadi Mei 12,
kuonesha shughuli mbalimbali za kitaaluma wanazozifanya wauguzi ikiwa ni
pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kiafya kama huduma ya mama na
mtoto, huduma za kupima VVU na ushauri nasaha.
Chama
cha wauguzi Tanzania (TANNA) ni chama kinachowawakilisha wauguzi na
wakunga wote Tanzania bara na Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein
Mwinyi.
0 comments:
Post a Comment