Na Janet Josiah
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kufanya
uzinduzi wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Mianzini, iliyopo
Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam, Mei 20.
Kata ya Mianzini inafanya uchaguzi mdogo kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wake, Cesylia Macha (CCM).
Akizungumza juzi, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jimbo la
Kigamboni, Yesaya Ibrahimu, alisema: “Maandalizi ya uzinduzi wa kampeni
yanaendelea vizuri, tunaendelea na mikutano midogo midogo ya jimbo…
Jumamosi tutafanya mkutano mkuu wa wilaya wenye agenda moja tu kuhusu
uchaguzi wa Kata ya Mianzini.”
CHADEMA imemsimamisha Cuthbert Ngwata kugombea udiwani wa kata hiyo katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Juni 16.
Kampeni kwa ajili ya chaguzi ndogo zimeshaanza Mei 15 mwaka huu baada
ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza kufanyika katika Jimbo la
Chambani, Pemba pamoja na kata 26 zilizopo katika halmashauri 21 nchini.
IMETOKA TANZANIA DAIMA LEO
0 comments:
Post a Comment