Habari hii imeandikwa na Baraka Mpenja, mmiliki wa blog hii na mwandishi wa mtanado wa FULLSHANGWE
Beki
wa Yanga Nadir Haroub “Canavaro” aliyeshika mwari baada ya kutangazwa
rasmi mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara uwanja wa taifa
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Habari ya
mjini bado nii ubingwa wa 24 wa Yanga ambao waliutwaa mapema kabla ya
ligi kumalizika, lakini furaha kubwa imekuja baada ya kuwafunga watani
zao wa jadi Wekundu wa Msimbazi Simba mabao 2-0 katika dimba la taifa
jijini Dar es salaam.
Jana
tulikuwa na mahojiano maalumu na kiungo kinda wa klabu ya Yanga, Frank
Domayo, leo hii mtandao huu umekutana na nahodha wa mabingwa hao wa ligi
kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013, Mzanzibar Nadir Haroub
“Canavaro” na mahojiano yameenda ifuatavyo.
FULLSHANGWE: Nahodha wa Yanga Nadir Haroub “Canavaro” umeiongoza klabu yako kutwaa ubingwa wa 24, unajisikiaje?
CANAVARO:
Aisee! nauchukulia kwa furaha kubwa sana, kiukweli mchezo ulikuwa mzuri
sana, tulicheza vizuri na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Watani
wetu wa jadi Simba.
FULLSHANGWE: Yanga mlistahili ushindi?
CANAVARO:
Kiukweli tulistahili, toka mwanzo wa mchezo mpaka mwisho tulicheza
vizuri sana, Simba walicheza kwa muda mfupi. Sisi tuliingia kwa lengo la
ushindi tu na tulicheza kuutafuta kufa na kupona ili kufurahia ubingwa
wetu na mashabiki wetu, tumefanikiwa!.
FULLSHANGWE: Wewe ni nahodha wa Yanga, siri ya kucheza vizuri zaidi ya Simba ilikuwa nini?
FULLSHANGWE:
Kikubwa ni umoja wa wachezaji wa Yanga, nimewaongoza na kuwasihi
tucheze kutafuta ushindi,wamenielewa vizuri. Ukumbuke tukiwa Pemba
tulifanya mazoezi kwa umoja mkubwa tukifirikia sana ushindi na
tumewashinda Simba.
FULLSHANGWE: Unawazungumziaje Simba?
CANAVARO:
Simba ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri, binafsi nawaheshimu sana ila
jana tuliwazidi sana na huo ndio mpira wa miguu, lazima ukubali
matokeo. Tuliwazidi kila Idara na hatuwapa nafasi zaidi ya penati
waliyopapa ingawa kipa wetu alicheza na tukaendelea na mchezo.
FULLSHANGWE: Baada ya mwamuzi Martin Saanya kutoa Penati ulimzonga sana, kwanini?
CANAVARO:
Sidhani kama ilikuwa sahihi, Mwamuzi ndio mtu wa mwisho na mimi ni
mchezaji, nitalalamika tu, lakini mwamuzi ndio mwisho. Mchezaji huna
ujanja mwamuzi atakapofanya maamuzi, nilikubali penati na kipa wetu
akaicheza vizuri sana.
FULLSHANGWE: Ulipewa Shampeni uifungue, baada ya kufanya hivyo ukainywa, unapenda pombe?
CANAVARO:
Daah! Sielewi nini kilitokea, mimi sio mlevi wala mvuta sigara,
nilijikuta kunywa baada ya furaha kuzidi. Leo hii nimemuomba msamaha
mama yangu kwa kitendo kile, nimekubali furaha inaweza kukusababisha
ukatenda dhambi na kumkosea Mungu, nimemuomba Mungu msamaha kwasababu
mimi sio mlevi wa pombe
FULLSHANGWE: Wewe haunywi pombe kabisa?
CANAVARO:
Sijawahi kunywa pombe na watu wanajua, furaha inapozidi mipaka inaweza
kukughraimu, nashangaa kwa kweli, Mungu namuamini sana, namtanguliza
mbele, anisamehe sana.
FULLSHANGWE: Ukikaa nafasi ya ulinzi huwa unaosha mipira bila kuremba, kwanini huwa una maamuzi ya haraka namna ile?
CANAVARO:
Duniani kote beki hasifiwi, unaweza kucheza vizuri na kupaka rangi
mipira na ukafanya kosa moja kuifungisha timu yako, utalaumiwa zaidi ya
ulivyocheza vizuri, mimi maamuzi yangu ni ya haraka sana, na ndio sifa
yangu kubwa. Hakika maamuzi kama yale huwa yananisaidia sana
kutoigharimu timu yangu.
FULLSHANGWE: Baada ya hapa unajiunga na timu ya taifa, unajisikiaje kutajwa na kocha Kim Paulsen katika kikosi cha Taifa stars?
CANAVARO: Nimefurahi sana! Suala
la timu ya taifa ni maamuzi ya mwalimu, cha msingi namshukuru kocha
kuniita. Timu ya taifa ni ya watu wote, mtu mwenye sifa anatakiwa
kuichezea, kikubwa ninawaomba Watanzania watuunge mkono katika safari
hii ya kuelekea Brazil mwakani, hatutawaangusha hata kidogo.
FULLSHANGWE: Asante sana Canavaro kwa ushirikiano, tutawasiliana zaidi!
CANAVARO: Asante sana kwa kunipa nafasi, wape salamu wana Yanga na karibu sana.
FULLSHANGWE: Asante na kila la heri!
0 comments:
Post a Comment