Taarifa
zilizotufikia katika chumba chetu cha habari zinasema kuwa msanii
maarufu wa Bongo Fleva Albert Mangwea amefariki dunia leo hii katika
hospitali ya St Hellen iliyoko South Africa, sababu za kifo chake
hazijatajwa mpaka sasa, ingawa redio nyingi jioni hii zinaeleza kuwa
chanzo cha kifo chake ni kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya.
Lakini
taarifa hizi hazijathibitishwa mpaka sasa, Mtandao huu unafanya
jitihada ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Ngwea
ili kujua ukweli wa taarifa ya kukumbwa na umauti.
Taarifa
hizi zimepokelewa kwa huzuni kubwa na watanzania nchini kote, jiji la
Dar es salaam limeshtushwa na taarifa hizo zinazotangazwa kwenye vyombo
vya habari, mitandao ya kijamii yaani blogs, Twita, n.k
Endelea kutembelea Mtandao huu wa MATUKIO DUNIANI kwa habari zaidi.
0 comments:
Post a Comment