Na Baraka Mpenja
Hivi
karibuni rais wa shirikisho la soka Tannzania, Injinia Leodigar Chila
Tenga alitangaza kutoa mipira mipya 1200 yenye thamani ya dola za
kimarekani elfu 30.
Mipira hiyo ililenga kuendeleza soka la Tanzania hususani soka la vijana.
Tenga alisema itanunuliwa mipira mipya na vituo vinavyotambuliwa na TFF vitapewa mipira hiyo.
Baadhi ya vyama vya soka mikoani vimegawa mipira 25 kwa kila kituo.
Lakini
swali kubwa ni aina ya mipira iliyotolewa, mfano kuna mipira yenye
nembo ya NMB, TFF na Malaria Haikubaliki, sasa hii mipira ya NMB
imenunuliwa wapi?
Au
hata NMB walitoa fedha kwa TFF kumsaidia Rais Tenga kununua mipira hiyo,
kama jibu ni ndiyo sio mbaya, lakini mbona kwenye mkutano na waandishi
wa vyombo vya habari hiyo haikusemwa?
Wenye
majibu ni vyama vya mikoa na viongozi wa TFF, mtandao huu unafanya
mawasiliano na viongozi wa mikoa yote na baada ya kupata majibu yao, TFF
watafuatwa ili kutoa ufafanuzi wa mipira hii.
0 comments:
Post a Comment