Na Baraka Mpenja
Mnamo
tarehe 22/04/2013 siku ya jumatatu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga alitoa mipira zaidi ya 1,200 yenye
thamani ya dola 30,000 za Marekani kwa vyama vya mpira wa miguu vya
mikoa ya Tanzania Bara na vituo 21 vilivyo hai vya kuendeleza vijana
(academies).
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) lilimpa Rais Tenga fedha hizo
ikiwa ni shukrani kwake kwa kushughulikia mgogoro wa uongozi wa mpira wa
miguu nchini Kenya uliodumu kwa miaka miwili; ambapo nchi hiyo kutokana
na mgogoro huo ilikuwa na vyama viwili (KFF na FKL).
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi mipira hiyo kwenye ofisi za TFF, Dar es
Salaam (Aprili 22 mwaka huu), Rais Tenga alisema amefanya hivyo kwa vile
anaamini kuwa mipira ndiyo kitu muhimu katika kuinua mchezo huo mahali
popote.
“Dhamira
yangi si kushukuru kwa hafla hii, bali kutoa sababu kwa nini nimefanya
hivi. Ninaamini kwa kuanzia mipira ndiyo muhimu, pili kwa kufanya hivi
itaonekana kweli mipira imegawiwa,” amesema Rais Tenga.
Vyama
vya mikoa ambavyo jumla ni 32 (Tanzania Bara na Zanzibar) kila kimoja
kimekabidhiwa mipira 25 (kumi saizi namba tano, 15 saizi namba nne kwa
ajili ya vijana). Kwa academies ambazo ni 21 kila moja imepewa mipira 25
(minane saizi namba tano, na 15 saizi namba nne).
Baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo wadau wa soka walimpongeza sana rais Tenga kwa kitendo hicho cha kusaidia soka la Tanzania.
Kutoa
mipira ni suala zuri na dhamira ya dhati ya Rais Tenga, lakini swali la
msingi hii mipira 1200 ilinunuliwa yote ama la, hilo ni swali muhimu
sana.
Tumezoea uchakachuzi wa masuala mbalimbali nchini Tanzania na kila mtu anajua wizi unaofanywa na viongozi wetu.
Mtandao huu umefanya jitihada za kufuatilia aina ya mipira iliyogawawiwa kwa vyama vya mikoa na vituo vya soka.
Ni
kweli maeneo ambayo mtandao huu umepita vituo vingi vimepata mipira
hiyo, je inakidhi vigezo na ndio ile waliyoonesha sampo pale TFF? Hilo
ni suala lingine.
Wakati
Tenga akizungumza na waandishi wa habari Aprili 22 mwaka huu kuhusiana
na kutoa mipira hiyo, hakika alisema ameamua kutumia dola elfu 30
alizopewa na FIFA kama zawadi kununua mpira mipya.
Hakusema kama kuna mipira ambayo ipo TFF ambayo itachanganywa na mipira mipya atayonunua kwa kiasi cha fedha alizotaja.
Wakati
kamera zetu zinahaha huku na kule kuangalia ufanisi wa zoezi la ugawaji
wa mpira, hakika tumeona mipira ya aina yake ambayo inaonekana katika
picha hizo hapo juu.
Kuna
mipira ina nembo ya NMB, Malaria na TFF, swali la msingi , hii mipira
imenunuliwa wapi?, Je kuna duka la NMB linalouza mipira au hii mipira
imetolewa wapi ili ipelekwa mikoani.
Katika
mikoa ambayo imechunguzwa ipatayo minne kuna tatizo la mipira hiyo,
mingine inaonekana na ya zamani na inachanika ovyo ovyo, sasa ndio
mipira aliyonunua Tenga?.
Baadhi
ya vituo vilishukuru na kusema kuwa hata vingepewa mipira mibovu kiasi
gani, zawadi ni zawadi, sawa wanaweza kuwa sahihi, lakini aliyetoa
zawadi alisema atatoa zawadi mbaya, lahasha Tenga hawezi kufanya hivyo,
sasa imekuwaje?.
Mtandao
huu unaendelea kufanya uchunguzi wa Mipira katika mikoa mbalimbali
baada ya hapo utatoa majibu ya mipira hiyo ambayo kuna fununu kuwa
inatofautiana na baadhi ya mipira iliyotolewa jijini Dar es salaam.
Kama TFF walichanganya mipira ya zamani na mipya, kwa sasa jibu la moja kwa moja halipo, kinachosubiriwa ni tafiti za mikoani.
Majina
ya viongozi wa vituo ambao ndio waathirika wa mipira hiyo tunayo na
mahojiano yao, lakini tunaendelea na utafiti, mambo yakikamilika tutatoa
jibu lake, endelea kufuatila mtandao huu ili ujue ukweli juu ya mipira
hiyo.
0 comments:
Post a Comment