RAFAEL BENITEZ: KOCHA BORA WA MWEZI APRIL 2013.
Shirikisho la mpira wa miguu nchini UINGEREZA FA,
limemtangaza meneja wa muda wa klabu ya CHELSEA , RAFAEL BENITEZ kuwa kocha
bora wa mwezi wa Aprili msimu huu kwenye ligi kuu ya nchini humo baada ya timu
yake kushinda michezo mitatu mfululizo
dhidi ya Sunderland, Fulham na Swansea,
huku ikitoa sare ya magoli 2-2 dhidi ya klabu ya LIVERPOOL kwenye mchezo uliopigwa dimbani ANFIELD mwezi uliopita.
Rafael Benitez |
Akiongea kupita mtandao wa klabu hiyo hiyo BENITEZ amesema siri ya mafanikio katika klabu
yake ni umoja na ushirikiano wa hali ya juu uliopo kati ya wachezaji , kocha na
viongozi wa timu kwa ujumla huku akisisitiza kuwa licha ya kushindwa kunyakua
ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu, bado timu yake ina nafasi kubwa
ya kufanya vizuri kwa msimu mwingine ujao kwani
kwa sasa wako katika nafasi
nzuri kwenye msimamo wa ligi ligi.
Hata hivyo Chelsea ambao wamejihakikishia tiketi ya kucheza
fainali ya kombe la shirikisho barani ulaya baada ya hapo juzi kuwatandika FC BASEL magoli 3-1 dimbani Stamfordbrige, kwa sasa
wako nafasi ya tatu alama moja mbele ya Arsenal kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa wamebakiwa
na michezo minne mkononi.
ARSENE WENGER;NINA MAPENZI YA KWELI NA ARSENAL.
Kocha wa klabu ya ARSENAL , ARSENAL WANGER leo ameweka wazi kuwa anapenda kubaki dimbani EMMIRATE kuendelea kufundisha klabu yake ya sasa licha ya kuwepo na tetesi kuwa klabu ya PARIS SAINT GERMAIAN ya huko nchini Ufaransa inamipango ya kumsajii mwishoni mwa msimu huu.
WENGER ambaye timu yake inang’ang’ana kubaki kwenye nafasi
ya nne bora kwenye msimamo wa ligi kuu
nchini Uingereza, akiongea na wanahabari amesisitiza kuwa ana mapenzi makubwa
na klabu ya Arsenal, hivyo haoni sababu ya kuhamia klabu nyingine kwa sababu ya
pesa huku akisaliti klabu yake anayoipenda
kwa moyo.
Kusho, Arsene Wenger, Jack Wilshere wakijadili jambo mazoezini. |
Aidha WENGER ameongeza kuwa licha ya klabu yake kupita katika kipndi kigumu cha ligi, bado anaamini
timu yake iko katka nafasi nzuri kwa
ajili ya msimu mwingine ujao.
MOURINHO: REKODI YANGU INAJIELEZA YENYEWE.
Kocha wa klabu ya
REAL MADRID JOSE MORINHO mapema leo akiongea na wanahabari, amesema
kuwa ni vyema watu wamzungumzie kwa kutumia kigezo cha mafanikio alionayo
kuliko kutumia kutumia kigezo cha
kushindwa kuchukua ubingwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Jose Mourinho. |
MORINHO mwenye asili ya nchini URENO,
aliwahi kushinda mataji manne katika nchi nne tofauti , lakini pia ni
miongoni mwa makocha watatu pekee waliowahi kunyakuwa ubingwa wa CHAPIONS LEAGUE akiwa na timu mbilli tofauti.
Hata hivyo kibabu huyo ambaye kwa sasa anahusishwa na taarifa za kuhamia klabu yake ya zamani ya CHELSEA
mwishoni mwa msimu huu, ameendelea
kusitiza kuwa rekodi ya ligi bado
inabaki kuwa yake licha ya mambo kumuendea kombo msimu huu kwenye hatua ya nusu fainali ya klbu bingwa
baada ya kutolewa nje ya michuano hiyo na klabu ya BORUSSIA DORTMUND kwa tofauti ya
goli 1-0
Kivuyo Francis www.goal.com
0 comments:
Post a Comment