Mafanikio haya yanakuja saa kadhaa baada
ya kocha wa Manchester United, Alex Ferguson kusema Benitez ndiye mtu
pekee anayemvutia akiwa kazini Stamford Bridge.
Robin van Persie ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kwa mara ya pili msimu huu, baada ya kushinda pia na Desemba.
Mjuzi: Rafael Benitez amechaguliwa kocha bora wa April Ligi Kuu England
Mkali wa wakali: Robin van Persie ameshinda tuzo ya tano ya Mchezaji Bora wa Mwezi
TUZO ZA BENITEZ KOCHA BORA MWEZI
Novemba 2005 - Liverpool
Desemba 2005 - Liverpool
Januari 2007 - Liverpool
Oktoba 2008 - Liverpool
Machi 2009 - Liverpool
Aprili 2013 - Chelsea
Mara ya mwisho kocha wa Chelsea kushinda
tuzo hiyo ilikuwa ni Aprili mwaka 2011, ilipochukuliwa na Carlo
Ancelotti kabla hajatupiwa virago na klabu.
Pamoja na kukandiwa sana na mashabiki wa
Chelsea, Benitez ameendelea kufanya vizuri sasa akiwania nafasi ya tatu
katika Ligi Kuu na tayari ameiwezesha timu kutinga fainali ya Europa
League kwa kishindo.
WACHEZAJI BORA WA MWEZI 2012/2013
Steven Fletcher (Sunderland) - Septemba
Juan Mata (Chelsea) - Oktoba
Marouane Fellaini (Everton) - Novemba
Robin van Persie (Man United) - Desemba
Adam le Fonde (Reading) - Januari
Gareth Bale (Tottenham) - Februari
Jan Vertonghen (Tottenham) - Machi
Robin van Persie (Man United) - Aprili
Muuwaji: Van Persie bao lake la mwisho alifunga kwa penalti dhidi ya klabu yake ya zamani, Arsenal
MAKOCHA BORA WA MWEZI 2012/2013
David Moyes (Everton) - Septemba 2012
Alex Ferguson (Man United) - Oktoba 2012
Steve Clarke (West Brom) - Novemba 2012
Andre Villas-Boas (Tottenham) - Desemba 2012
Brian McDermott (Reading) - Januari 2013
Andrew Villas-Boas (Tottenham) - Februari 2013
David Moyes (Everton) - Machi 2013
Rafael Benitez (Liverpool) - Aprili 2013
0 comments:
Post a Comment