Tangu alipoingia Chelsea kama kaimu mkufunzi Rafael Benitez amekuwa na wakati mgumu kwani mashabiki wa Stamford Bridge wamekuwa hawampendi.
Lakini baada ya kuifunga Benfica mashabiki
hao hao ambao walikuwa hawampendi Benitez waliishangilia ushindi wa timu yao
kwa vifijo na nderemo huku wakisahau chuki waliokuwa nao kwa kaimu meneja huyo.
Hatimae kocha Mhispania Rafael Benitez ataondoka Chelsea akiwa na
tabasabu baada ya timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Europa League kwa
kuifunga timu ya Benfica ya Ureno 2-1 usiku wa Jumatano katika uwanja wa
Amsterdam, Uholanzi.
Hii ni baada ya Branislav Ivanovic kufunga
bao la pili maridadi kwa kichwa wakati dakika
za majeruhi wakati mashabiki wakiamini
mechi ingeongezwa dakika 30 za nyongeza na pengine ingeamuliwa kwa mikwaju ya
penati ya piga nikupige,lakini haikuwa hivyo.
Mwaka jana Chelesea ilishinda Kombe la Klabu
bingwa bara Ulaya na mwaka huu wamebeba kombe la Europa League.
Bao lakwanza la Chelsea lilifungwa na
mshambulizi Fernando Torres nao Benfica wakapata lao kupitia mwaju wa penalti
uliofungwa na Oscar Cardozo.
Ushindi wa Chelsea unamfanya Rafael Benitez
kuwa meneja wa nne kushinda kombe la Klabu Bingwa Uropa na la Europa League
zaidi ya mara mmoja.
Wengine
amabo wamewahi kushinda kumbe hilo zaidi ya mara moja ni Giovanni Trapattoni:
1977 (Juventus); 1991 (Inter); 1993 (Juventus) ,Luis Molowny: 1985 & 1986
(Real Madrid) Juande Ramos: 2006 & 2007 (Sevilla).
0 comments:
Post a Comment