Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya kuisaidia Chelsea kutwaa ndoo ya ligi ya Uropa na leo hii kuwaponda
wale wote waliokuwa wanamponda kuwa hawezi kufanya lolote, kocha
Mhispania Rafa Benitez sasa milango ipo wazi kujiunga na klabu ya
Everton ili kurithi mikoba ya kocha aliyetimukia Manchester United David
Moyes.
Benitez
aliyeiongoza Liverpool katikati ya 2004 na 2010 atajikuta hana kazi
mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa kuifundisha Chelsea kwa
muda kumalizika, huku mmiliki wa klabu hiyo Bilionea Roman Abramovich
akimpotezea bila kumuongezea mkataba licha ya kuwapa mafanikio msimu
huu.
Licha
ya taarifa kuzagaa katika vyombo vya habari kwamba anakaribishwa
Everton, Benitez alisema “Ninaiheshimu sana Everton. Wamefanya kazi
nzuri sana mwaka uliopita, na lazima niwape sifa. Lakini nafikiri
itakuwa ngumu kwangu mimi kwenda Goodison Park, pia itakuwa ngumu kwao
kuja kuongea na mimi, hata mimi ni ngumu kwenda klabuni hapo”.
Wakati
Benitez akiongea hayo, mkongwe wa wekundu wa Anfield ama majogoo wa
jiji, Lejendari Jamie Carragher alisema kocha huyo anaweza kurudi
Merseyside kuwanoa Liverpool.
Alipoulizwa
kama anaweza kujiunga na Everton, Carragher ameimbia talkSPORT, kwanini
hapana?. Wanamtafuta kocha na Benitez anatafuta kazi na anataka kukaa
ligi kuu soka nchini England, anapenda ligi hii sana.

Benitez
akishangilia baada ya kutwaa mzigo ama kombe la ligi ya Uropa katika
uwanja Amsterdam nchini Uholanzi katikati ya wiki hii

MIAKA YA NYUMA: Benitez na Carragher katika mazoezi ya majogoo wa jiji mwaka 2007

Benitez akiwa na kocha wa Everton David Moyes anayetimukia United baada ya kibabu Fergie kustaafu msimu huu utakapomalizika mei 19 mwaka huu
0 comments:
Post a Comment