Na Baraka Mpenaja
Wakati
timu za ligi kuu Tanzania bara zikiangaza darubini zao kusaka wachezaji
wapya wa kuwasili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara,
mlinzi wa kushoto wa klabu ya maafande wa jeshi la kujenga taifa JKT
Ruvu ya mkoani Pwani Stanley Nkomola amejipigia debe kwa klabu za Simba
na Yanga akitaka zimsajili kwa msimu ujao wa ligi.
Nkomola ameiambia MATUKIO DUNIANI
kuwa kama timu hizo zinataka kumsajili kwa dau nono yupo tayari
kuachana na wapiga kwata hao wanaonolewa na kocha mkongwe Keny
Mwaisabula “Mzazi”.
“Natamani
kufika mbali zaidi kisoka, nataka kucheza kimataifa, nafikiri Simba na
Yanga ni timu nzuri sana, zinaweza kunifikisha ninapotaka”. Alisema
Nkomola.
Alipoulizwa
kama ataweza kuhimili ushindani wa namba katika klabu hizo, Nkomola
alijigamba na kusema kuwa Tanzania ya sasa hakuna beki bora wa kushoto
kama yeye.
“Hakuna
mwalimu anayeweza kumnyima nafasi mchezaji anayecheza vizuri, najiamini
sana, naweza kushindana katika klabu yoyote hapa Tanzania na kucheza
kikosi cha kwanza muda wote”. Alisema Nkomola.
Beki huyo kisiki alisema kama hatapata timu kubwa kwa sasa ataendelea kuitumikia klabu yake ya sasa kwa msimu ujao wa ligi.
“Nafurahi
sana kucheza JKT Ruvu kwa sasa, timu ina morali kubwa na wachezaji
wazuri, lakini soka ni ajira kwa sasa, kama Simba na Yanga watanihitaji
sioni tatizo kujiunga na timu hizo zenye majina makubwa nchini
Tanzania”. Alisema Nkomola.
Akizungumzia
jinsi walivyomaliza ligi, Nkomola alisema walicheza kwa morali kubwa
mechi za lala salama ili kukwepa mkasi wa kushuka daraja, na kama
wangezembea wangekwenda na maji.
“Timu
ilijengwa vizuri sana dakika za mwisho, kocha mpya Mwaisabula alitutaka
kucheza kwa lengo la kubakia ligi kuu ili tujipange vizuri msimu ujao,
tulijitahidi sana kuhakikisha tunafanya kama alivyotuagiza na
kufanikisha ndoto zetu, sasa tunakuja msimu ujao kwa kasi kubwa”.
Alisisitiza Nkomola.
0 comments:
Post a Comment