Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya wekundu wa kusini mwa Ujerumani, `The Bavarian`, Bayern Munich na
mabingwa wa Bundesliga msimu wa 2012/2013 kutwaa ubingwa wa ligi ya
mabingwa barani ulaya usiku wa kuamkia leo kwa kuwatandika Nyuki wa
kaskazini mashariki mwa nchi hiyi Borussia Dortmund mabao 2-1, wamepiga
bonge la sherehe na kuwaacha Waingereza wakiduwaa katika ardhi yao.
Arjen
Robben aliyetoa pasi ya bao la kwanza katika mchezo huo na kutia
kimiana bao la pili na la ushindi kwa klabu hiyo, aliungana na wachezaji
wenzake katika Hoteli ya Grosvenor House Park Lane kushangweka.
Bayern
waliingia uwanjani wakiwa na machungu ya kupokonywa tonge mdomoni msimu
uliopita baada ya Chelsea kuwafunga katika dimba lao la Allianz Arena
kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Katika
sherehe hizo, Bastian Schweinsteiger, aliyekosa penati msimu uliopita
alionekana mwenye furaha zaidi huku akijifunga kitambaa `skafu` kichwani
na kuwaongoza wenzake kushangilia ubingwa wao.
Jupp
Heynckes mwenye miaka 68 alijumuika na mashabiki wengi wa klabu yake
kushangilia ubingwa wake wa pili katika msimu huu kwa maana ya
Bundesliga akiwapokonya wapinzani wao Borrusia Dortmund na UEFA
aliyotwaa jana usiku.
Wachezaji
wa Bayern Kama wanajua vile, walisafiri na wapenzi wao pamoja na wake
ili kushangilia pamoja taji la UEFA na hatimaye hapo jana wakafanikiwa
kutimiza ndoto zao huku Robben akidondosha machozi mbele ya umati mkubwa
wa mashabiki wa klabu yake kutokana kuukosa ubingwa huo mara nyingi.
UFUNGUZI
WA BURUDANI: kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes (kushoto) akifungua
burudani kubwa ya kushangilia ubingwa huku akisaidia na kiungo fundi
Bastian Schweinsteiger
MWISHO WA YOTE AMESHINDA: Schweinsteiger akiwa amebeba ndoo ya UEFA pembeni akiwa na kimwari wake Sarah Brandner
SHANGWE KUBWA: Arjen Robben (kulia) na Mario Mandzukic (katikati) akiungana na Schweinsteiger
NJOO HAPA: Uli Hoeness akipongezwa na Schweinsteiger katika hoteli Park Lane
MWENDO WA PICHA: Schweinsteiger akipiga picha kupitia simu yake ya mkonononi
WACHEZAJI
WA AKIBA: Xherdan Shaqiri, Anatoliy Tymoshchuk na Rafinha hawakuanza
mechi ya jana, lakini walijiunga na wenzao kushangilia ubingwa wao
HADI WEWE?: Mkurugenzi mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge akionesha utaalamu wake wa kusakata muziki, hadi raha
Shabiki wa Bayern akionesha umahiri wake wa kucheza baada ya kutwaa tajil lao
FURAHA KUBWA: Wachezaji wa Bayern wakiimba wimbo wa kushangilia ubingwa huku wakiongozwa na Schweinsteiger pamoja na Robben
0 comments:
Post a Comment