Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hakika
Wajerumani si mchezo katika soka, fainali ya ligi ya mabingwa barani
ulaya imepigwa katika dimba la Wembley jijini London usiku huu ambapo
kwa mara ya kwanza timu mbili kutoka Ujerumani zimekutana katika mechi
kali na ya kusisimua baina ya wekundu wa kusini mwa ujerumani Bayern
Munich na nyuki wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo Borrusia Dortmund.
Ilikuwa bonge la mechi, kiukweli ni moja ya fainali nzuri kuwahi kutokea katika historia ya fainali ya UEFA.
Kwa
kawaida mechi nyingi za fainali huwa zinapigwa mpaka dakika 120 mpaka
mikwaju ya penati kama ilivyokuwa kwa mwaka jana ambapo Chelsea
waliifunga Bayern, lakini fainali ya leo imepigwa ndani ya dakika
tisini.
Winga
hatari wa FC Bayern Mholanzi Arjen Robben ameipatia klabu yake zawadi
kubwa sana ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kufunga bao la pili na
la ushindi katika dakika ya 88 ya kipindi cha lala salama.
Bao
hilo limetokana na kazi nzuri ya winga mwenye kasi zaidi Frank Ribery
aliyempa pasi nzuri Robben na kupachika bao kiufundi zaidi.
Ubingwa leo ni watano kwa Bayern ambao katika misimu minne wamecheza mechi tatu za fainali bila mafanikio.
Bao
la Robben limemfanya atoe machozi kutokana na kuwa na kumbukumbu ya
kupoteza penati msimu wa mwaka jana na kuwanyima ubingwa Bayern, lakini
leo bao lake limekuwa dhahabu kubwa sana kwa mashabiki wa klabu yake.
MABINGWA WAPYA: Bayern Munich wamefanikiwa kuwa mabingwa mara tano wa UEFA baada ya kuwakwanyua Borrusia Dortmund usiku huu.
Ni shangwe kubwa sana kwa wachezaji wa Bayern baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA usiku huu
Robben akinyanyua mwari wa UEFA, hakika ametafuta sana
ILIKUWA
NAFASI NZURI: Kipindi cha kwanza kipa Roman Weidenfeller wa Borrusia
alimnyima Robben nafasi ya kufunga wakati huo huo Manuel Neuer wa
Bayerna nae alimnyima nafasi ya kufunga Robert Lewandowski
Robben alipoteza nafasi moja muhimu sana kipindi cha kwanza baada ya kupiga mpira na kumgonga kipa usoni bila kutegemea
MATATA: Franck Ribery alipona kupata adhabu baada ya kuonekana baada ya mkono wake kumpiga Lewandowski katika paji la uso
Robben akishangilia bao lake la ushindi usiku huu
0 comments:
Post a Comment