RAIS
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, (TEC), Tarcisiuus Ngalekumtwa
amewataka wanafunzi nchini kuweka hekima mbele hali itakayowasidia kuwa
viongozi waadilifu katika jamii hapo baadaye.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Rais huyo, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la
Iringa Mijini, wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya kutimiza miaka 25
tangu kuasisiwa kwa shule ya Sekondari Montfort, iliyoko Rujewa mkoani
Mbeya.
Akizungumza
na MATUKIO DUNIANI kwa njia ya simu, kwa niaba ya Rais huyo, Mkuu wa Shule
hiyo, Ansgar Kigane, alisema Taifa lolote ili lisonge mbele
kimaendeleo linahitaji kuwa na wanafunzi waliyojengeka kimaadili.
Alisema
wanafunzi wa ngazi zote wanapaswa kuweka hekima mbele kitendo ambacho
kitawasidia katika kumtambua mungu ambaye atawaongoza katika kutenda
mema na kujiepusha na unyakuaji wa haki za wengine.
Rais
Ngalekumtwa, alisistiza kuwa wanafunzi wanapaswa kuzingatia kile
wanachofundishwa na wa walimu wao, lengo likiwa ni kuja kusimamia
rasilimali za nchi kwa usawa na kulikomboa taifa hili kutoka kwenye
dimbwi la umasikini.
Naye
Mkuu wa Shule hiyo, Kigane, alisema tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka
1988, yapo mafanikio ya kujivunia kutokana na vijana wengi waliosoma
katika shule hiyo kushika nyadhifa mbambali katika baadhi ya sekta
tofauti nchini.
“Shule
yetu ilikuwa ikitoa elimu ya kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne
lakini sasa tumepiga hatua, tunatarajia Julai mwaka huu kufungua kidato
cha tano, haya nayao ni mafanikio ya kujivunia na shule yetu ni ya
mchipuo wa kilimo ambacho tunakisoma kwa vitendo kutokana kuwa na
mashamba ya mfano”alisema Kigane.
Alizitaja
changamoto kuwa ni kushuka kwa maadili kwa pande zote, kutoka kwa
wazazi na vijana ambao wengi siku hizi wamekuwa wakilelewa na mitandao
ya kijamii na vyombo vya habari kuliko wazazi, zaidi wakishika yale
machafu hali inayozidi kuchangia kushuka maadili ya vijana nchini.
Kigane
alisema katika kupambana na upotofu huo shule imejipangia utaratibu wa
kutoa semina kwa wanafunzi kila wiki katika madarasa yao lengo likiwa ni
kuwaelimisha kuhusu faida na hasara za undawazi, ambako anaamini
inaweza kuleta mabadiliko.
0 comments:
Post a Comment