Na Baraka Mpenja Kwa msaada wa Sportsmail.com
Msimu
wa ligi kwa nahodha machachari wa majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool,
Steven Gerrard umefikia ukingoni baada ya kuthibitishwa kuwa nyota huyo
anafanyiwa upasuaji sehemu ya bega wiki hii.
Gerrard
alitakiwa kufanyiwa upasuaji baada ya msimu kumalizika lakini klabu
yake imesema imeamua kumfanyia zoezi hilo baada ya majeraha yake
kuendelea kuwa makubwa.
Zoezi
hilo la upasuaji litamfanya nyota huyo kukosa michezo miwili ya ligi
kuu Engalanda na mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Uingereza
dhidi ya Brazil mwezi ujao, pia atakosa mchezo dhidi ya Jamhuri ya
Ireland mei 29 mwaka huu uwanjani Wembley.
Gerrard
itahitaji miezi sita hadi nane kupona na Liverpool inatarajia kumtumia
katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu.
Msimu wa ligi kwa Gerrard umefikia tamati
Ratiba ambayo Gerrard atakosa
May 12 – Fulham v Liverpool
May 19 – Liverpool v QPR
May 21 – Ajax Cape Town v Liverpool
May 29 – England v Republic of Ireland
June 2 – Brazil v England
May 19 – Liverpool v QPR
May 21 – Ajax Cape Town v Liverpool
May 29 – England v Republic of Ireland
June 2 – Brazil v England
Liverpool walitangaza jana kuwa watacheza mechi ya kirafiki ya kumalizia msimu dhidi ya Ajax Cape Town.
Kupona: Baada ya wiki sita hadi nane na ataonekana katika maandalizi ya ligi kuu England Msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment