Mbunge
wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu (kushoto) akijadiliana jambo
nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo na Mbunge wa Jimbo la Iringa
Mjini Peter Msigwa(katikati) na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini
, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu.
Picha na Magreth Kinabo -MAELEZO
Baadhi
wa askari polisi, magereza na uhamiaji wakiwa katika viwanja vya Bunge ,
mjini Dodoma mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk.Emmanuel Nchimbi akitoka nje ya ukumbi wa Bunge leo mara baada ya
kuwasilisha hotuba yake ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara
yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.Emmanuel Nchimbi akitoka nje ya ukumbi
wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya
makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake mwaka wa fedha 2013/2014
na kauli ya serikali kufuatia mlipuko wa bomu mjini Arusha. Kushoto ni
Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijika
na kulia ni Mbunge wa Jimbo Kigoma Kusini, David Kafulila.
0 comments:
Post a Comment