Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Baada
ya kipute cha jana baina ya Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund
kumalizika kwa Madrid kushinda kwa mabao 2-0 na kutolewa kwa wastani wa
mabo 4-3 kufuatia kipigo cha 4-1 nchini Ujerumani, leo ni leo tena
ambapo FC Barcelona wanahitaji kufuta kipigo cha 4-0 Allianz Arena
katika mchezo wa leo usiku dimba la Camp Nou.
Katika
mchezo wa jana usiku nyota wa Madrid Mreno Cristiano Ronaldo alishindwa
kuibeba timu yake katika dimba la Santiago Bernabeu, leo pia macho ya
mashabiki wa soka duniani ni juu ya mchezaji bora wa FIFA mara nne
mfululizo Lionel Andrew Jorge Messi ambaye atawaongoza wakatalunya
kufuta kipigo kizito cha 4-0 kutoka kwa wekundu wa kusini mwa ujerumani,
FC Bayer Munich.
Mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani Lionel Messi ndio tegemeo kubwa kwa Barca leo hii kufuta kipigo kutoka kwa Munich.
Sergio Busquet hali yake ipo mashakani kucheza mchezo wa leo kufuatia kusumbuliwa na majeruhi
KAZI ISIYOWEZEKANA: Barca wamejiandaa kushinda na kucheza fainali leo
AKIWA NA PRESHA: Kocha wa Barca Tito Vilanova sijui kama ataweza kufuta kipigo cha mchezo wa kwanza
WATU HATARI SANA: Lionel Messi na Alexis Sanchez wanatarajia kuibeba Barca mbele ya Bayern
WATU HATARI SANA: Lionel Messi na Alexis Sanchez wanatarajia kuibeba Barca mbele ya Bayern
MABADILIKO: Alex Song anaweza kuanza endapo Busquets hatakuwa fiti kabisa
Xavi ana wajibu mkubwa wa kusiadia timu yake leo
WACHEZAJI WENYE VIPAJI VIKUBWA: Barcelona ndio timu bora zaidi barani ulaya kwa sasa
Gerard Pique anatakiwa kucheza kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile cha Ujerumani
Andres Iniesta ni moja kati ya wachezaji wenye vipaji vikubwa zaidi duniani
0 comments:
Post a Comment